Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo inatarajia kuwakutanisha Maafisa Utamaduni na Michezo lengo ikiwa ni kujadili mikakati bora ya kuendeleza sekta hizo.
Akizungumza Mei 06,2021 katika mahojiano na Kituo cha Redio cha A FM Jijini Dodoma Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo nchini, Yusufu Singo ameeleza kuwa kikao hicho kitakua cha siku mbili na kitaongozwa na mada mbalimbali pamoja na kujadili utekelezaji wa Sera,Kanuni na Miongozo mbalimbali ya Sekta hizo.
Hata hivyo, Mkurugenzi huyo alitumia nafasi hiyo kueleza kuwa maandalizi ya Mechi ya Simba na Yanga itakayochezwa Mei 08,2021 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa yamekamilika.
“Habari na Michezo ni Sekta zinazotegemeana sana kwa mfano mwisho wa juma hili tuna mechi ya Simba na Yanga, bila umma kuelezwa vizuri juu ya mechi hii inaweza kukosa msisimko” amesisitiza Mkurugenzi Singo.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment