MFANYABIASHARA KIZIMBANI KWA KUTISHIA KUUA KWA BASTOLA | Tarimo Blog

FANYABIASHARA, Adelard Lyakurwa (58), anayefanya shughi uli zake Kariakoo amepandishwa katika kizimba cha  Mahakama ya Wilaya ya Ilala  kujibu shtaka moja la kutishia kumuua mfanyabiashara mwenzie marufu, Valence Lekule  kwa silaha,  Bastola 

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa Serikali, Aziza Mhina  mbele ya Hakimu Mfawidhi Martha Mpaze, imedai, Julai 30,2020 huko katika maeneo ya Kariakoo katika mtaa wa Mbaruku na Swahili iliyopo Wilaya ya Ilala Mkoani Dar ss Salaam,  mshtakiwa Lyakurwa akiwa na lengo la kuua, alimtishia Valence Lekule kumuua kwa kutumia bastola huku akijua kuwa kufanya hivyo ni kosa na ni kinyume na kifungu cha 89 (2)(a) cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2019.

Hata hivyo, mshtakiwa Lyakurwa amekana kutenda kosa hilo na amerudishwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ambapo mahakama imemtaka kuwa na wadhamini wawili ambao watakuwa na barua zinazotambulika kisheria na kusaini bondi ya Sh. Milioni moja.

Kwa mujibu  wa upande wa mashtaka upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na wameomba ipangiwe tarehe nyingine kwa ajili ya kumsomea mshtakiwa maelezo ya awali.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 2,2021 itakapokuja kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali.


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2