MREMBO FILBERTHA ATEULIWA KUWANOA WALIMBWENDE WA MISS DODOMA | Tarimo Blog

MREMBO Filbertha Juma ameteuliwa na Kamati ya Miss Dodoma kuwa mkufunzi  wa kuwanoa walimbwende hao.

Akizungumza na Michuzi Tv Mara baada ya kuteuliwa amesema ni nafasi yake Sasa kuhakikisha kila mrembo atakaekuwa kambini anakua na nidhamu na mwenye kufuata maadili.

"Unapowakutanisha Wasichana kutoka sehemu mbalimbali tegemea kuona hata tabia zao kuwa tofauti naamini kila mtu anajielewa jukumu langu ni kuhakikisha nawapa Ushirikiano wa kutosha pamoja mafunzo yanayostahili."

Aidha, Mkufunzi huyo amezungumzia tabia ya wadau wa urembo kutokabidhi zawadi za warembo kwa wakati nakupelekea Tasnia ya urembo kuonekana ni ya utapeli .

"kwa upande wangu sijawahi kukumbana nayo ila napenda kusisitiza Sana kwa Wadau kukabidhi zawadi za washindi au Mshindi mapema kuliko kuvunjiana heshima sababu tukio Kama hilo linaichafua Sana tasnia yetu siku hadi siku wakati ni mojawapo ya ajira na inaajiri watu wengi na imeshatoa viongozi mbalimbali akiwemo Jokate,Chuchu hansy na wengine."

Aidha Filbertha amesema anategemea mashindano ya mwaka yatatoa warembo wenye weledi na sifa zote na wenye moyo wa kusaidia jamii kupunguza vitendo viovu na kutoa elimu ya kijinsi.


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2