MTANZANIA RAWAN DAKIK MBIONI KUVUNJA REKODI YA KUKWEA MLIMA EVEREST | Tarimo Blog






RAWAN Dakik (20) yupo mbioni kuvunja rekodi ya kuwa mtanzania wa kwanza mwanamke na kijana mdogo zaidi barani Afrika kupanda mlima Everest ambao ni  mrefu zaidi uliwenguni. Hadi sasa Rawan amefanikiwa kupanda mita 6,400 kwa siku nne pekee kutoka katika kambi  maalumu ya mlima Everest ambayo ipo mita 5,300 kutoka usawa wa bahari.

 Rawan ataanza mzunguko wa pili jumanne wiki ijayo ambapo atafikia mita 7,200 kwa siku tano.

Rawan ameeleza kuwa inachukua takribani miezi miwili kupanda mlima Everest ikiwa hali ya hewa inaruhusu kukwea mlima na kwamba amejipanga kumaliza kukwea mlima huo mrefu zaidi ulimwenguni wenye mita 8,850 kabla ya mwisho wa mwezi Mei.


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2