Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Dkt Leonard Chamuriho amesema ujenzi wa Meli ya Mv Mwanza Hapakazi tu ambao hadi sasa umefikia asilimia 74 utakamilika baadaye mwakani.
Waziri Chamuriho ameyasema hayo leo jijini Mwanza alipokuwa akikagua ujenzi wa meli hiyo ya kisasa inayojengwa na Kampuni ya Gas Ente kutoka Korea ya kusini ikishirikiana na Kaang Nam Corperation pamoja na Suma JKT.
Aidha Waziri Chamuriho amesema ujenzi wa meli hiyo ni moja ya miradi mikubwa minne inayotekelezwa na kampuni ya huduma za Meli Nchini (MSCL) na kusimamiwa na Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi.
“Miradi mengine inayotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa ni pamoja na ukarabati wa Meli ya New Victoria,Ujenzi wa MV Butiama pamoja na Chelezo ambayo ujenzi wake umekamilika”, amesema Chamuriho.
Katika hatua nyingine Waziri Chamuriho amesema Wizara pia imejipanga kuendeleza miradi mingine katika Ziwa Tanganyika na Ziwa Nyasa ikiwemo mradi wa Ukarabati wa meli kongwe ya MV Liyemba .
Kwa upande wake Msimamizi wa mradi wa ujenzi wa Mv Mwanza Mhandisi Vitus Mapunda amesema Ujenzi huo umeajiri Zaidi ya watumishi 180 katika kada mbalimbali na utakapokamilika utaleta fursa nyingi za ajira nchini.
Naye Kaimu Mtendaji Mkuu wa Huduma za Meli (MSCL) Philemon Bagambilana amesema kampuni imejipanga kuboresha na kutoa huduma bora katika usafiri wa majini kwenye Ziwa Victoria, Ziwa Nyasa, Ziwa Tanganyika na kupanua huduma kwenye Bahari ya Hindi.
Muonekano wa Meli ya Mv -Mwanza Hapa Kazi tu inavyoendelea kujengwa na hadi sasa ujenzi wake umefikia asilimia 74 na unatarajiwa kukamilika ifikapo mwaka 2022.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Dkt Leonard Chamuriho akipanda ngazi kwenda kukagua ujenzi wa Meli Mpya ya Mv Mwanza Hapa kazi tu ambayo ujenzi wake umefikia asilimia 74 na inatarajia kukamilika mwaka 2022 na itakapokamilika itakuwa na uwezo wa kuchukua abiria 1200 na mizigo tani 400.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Dkt.Leonard Chamuriho (wa katikati) akitoa maelekezo kwa wahandisi wanawake wanaoshiriki katika ujezi wa Meli Mpya ya Mv- Mwanza Hapa Kazi Tu.Mafundi wa kampuni ya Ges Entec ya Korea ya Kusini wakiendelea na kazi ya kuchomelea sehemu ya Nje ya Meli ya Mv Mwanza Hapa Kazi Tu, Ujenzi wa Meli hiyo unatarajiwa kukamilika Mwakani.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Huduma za Meli Nchini (MSCL) Bw, Philemon Bagambilana akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Dkt Leonard Chamuriho mara baada ya kukagua ujenzi wa Meli mpya ya Mv Mwanza hapa kazi tu.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment