*Fedha zitakazopatikana kwenda kwa watoto njiti
Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
SHIRIKA la Bima la Taifa (NIC) limekuwa mdhamini mkuu wa mbio za Bima marathon zitakazofanyika Mei 29 mwaka huu katika uwanja cha Mlimani City Jijini Dar es Salaam.
Marathon hizo zimelenga kukusanya fedha kwa ajili ya kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuzuia vifo vya watoto njiti na kuimarisha afya zao kwa fedha hizo kununua vitanda maalum.
Hayo yamebainishwa Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Mteja wa NIC Isaya Mwakifulefule wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na udhamini wa marathon hizo.
Amesema kuwa NIC wamekuwa mstari wa mbele kusapoti mambo mbalimbali yenye tija na lengo la kukuza ajira kwa vijana nchini na kulinda afya zao pamoja na kutengeneza mawasiliano ya wadau hivyo Bima Marathon wana lengo hilo kwa watoto njiti.
Amesema Kuna makusanyo yanayopatikana kwenye kujiandikisha kwenye hizi mbio, sehemu yake inakwenda kupelekwa kwaajili ya kufariji watoto waliozaliwa njiti katika wodi yao maalum.
"NIC tuliona kupitia mbio hizi tushiriki kuweza kusaidia watoto hawa kwani ni jamii ambayo inatakiwa kuangalia kwa karibu”. Amesema Mwakifulefule.
Mwakifulefule ametoa wito kwa watanzania kuendelea kujiandikisha kwa kujitokeza kwa wingi waje kushiriki mbio hizo kwani kushiriki kwao si tu watakimbia na kulinda afya zao lakini pia watasaidia watoto njiti waweze kufanikisha ndoto zao
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Bima Marathon Baraka Mtavangu amewashukuru NIC kwa kuweza kuwa wadhamini wao katika mbio hizo hivyo wamekuwa na mchango mkubwa hasa katika kuleta tabasamu kwa watoto njiti ambao ni Taifa la leo.
Hata hivyo amesema washiriki wote watakaoshiri watepewa tshirt na medali pamoja na mshindi wa kwanza atapewa milioni moja, mshindi wa pili atapewa laki saba na mshindi wa tatu atapewa laki tano hii ikimaanisha kwamba washindi wa kiume na washindi wa kike tuti ya kilometa 10 na kilometa 21.
“Katika kilometa 5 zawadi zote ambazo tumeziweka kwa mshindi wa kwanza atapewa laki mbili, mshindi wa pili laki moja na mshindi wa tatu 50,000 hii ni kwa watoto ambao watakuwa wamekuja kukimbia ama kutembea kwenye kilometa tano”. Amesema Mtavangu.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment