PROF. MKUMBO AKIPONGEZA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM KWA KUBUNI UTARATIBU WA MASHINDANO YA UBUNIFU NA UJASIRIAMALI. | Tarimo Blog

Na Eliud Rwechungura

Waziri wa Viwanda na Biashara, Prof. Kitila Mkumbo amekipongeza Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kubuni utaratibu wa mashindano ya wanafunzi ya Ubunifu na Ujasiriamali inayofanyika kila mwaka.

Prof. Mkumbo ameyasema hayo Mei 08, 2021 katika siku ya wanafunzi ya Ubunifu na Ujasiriamali na fainali za Ubunifu na Ujasiriamali Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika ukumbi wa Nkrumah iliyokuwa na kauli mbiu inayosema “Badili Changamoto kuwa Fursa”

“Nakipongeza Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kubuni utaratibu kama huu wa kusaidia kuibua na kukuza vipaji vya ubunifu vya vijana wetu katika kujibu matatizo ya jamii. Mimi hapa ni nyumbani, hivyo najisikia vizuri kuwepo hapa na kushiriki pamoja nayi” ameeleza Prof. Kilila Mkumbo

Prof. Kitila ameeleza kuwa ujuzi unaotakiwa katika soko la ajira na nini wanafunzi wafundishwe ili wakubalike katika soko la ajira lina mjadala mrefu duniani kote. 


Prof. Kitila amesisitiza kuwa tafiti zinaonesha kuwa mataifa yaliyoendelea kama Marekani na Ulaya yameingiza elimu ya ujasiriamali katika mitaala yao zaidi ya miaka kumi iliyopita na kuleta matokeo chanya katika kuongeza fursa za wahitimu kupata ajira, kujiajiri, kutoa michango katika usitawi wa jamii na kukuza uchumi.

Aidha, Prof Mkumbo wamewahakikishia mojawapo ya vipaumbele vya muhimu kabisa katika Wizara anayoiongoza ni kufanya kazi kwa nguvu zote ili kuhakikisha kwamba haiwakatishi tamaa vijana wenye mawazo ya ubunifu.



Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2