Na Victor Masangu, PWANI
SERIKALI ya Mkoa wa Pwani katika kuhakikisha inatekeleza kwa vitendo azma ya kuwa na uchumi wa viwanda na kuwapa fursa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi imekutana na baadhi Wawakilishi (Delegation) kutoka Chemba ya Wafanyabiashara wa Kichina Tanzania (Chinese Business Chamber in Tanzania) kwa lengo la kujadili na kupanga mikakati ya kupata ardhi kwa ajili ya ujenzi wa viwanda.
Katika kikao hicho ambacho kiliongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani na kuhudhuliwa na baadhi ya viongozi mbali mbali wa Mkoa lengo ikiwa ni kufanya mazungumzo na wawakilishi hao kwa ambayo yataweza kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo kupitia sekta ya uwekezaji wa viwanda mbali mbali ambavyo vikikamilika vitaweza kuwa mkombozi mkubwa kwa wananchi katika kutoa fursa za ajira na kukuza uchumi.
Akizungumza katika kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo alibainisha kwamba lengo kubwa la ujio wa wawakilishi hao ni kuweza kutafuta eneo la ardhi kwa ajili ya Ujenzi wa Viwanda ikiwa ni kutekeleza maombi waliyowasilisha kwa Mhe Rais walipokutana na kufanya mazungumzo Aprili, 21 mwaka 2021.
“Tumepokea ugeni huu na katika mazungumzo yao ujumbe huo umekuja kwa lengo kutafuta Ardhi kwa ajili ya Ujenzi wa Viwanda ikiwa ni kutekeleza maombi waliyowasilisha kwa Mhe Rais walipokutana na kufanya mazungumzo hivi karibuni kwa hiyo sisi kama Mkoa wa Pwani suala hili tutalifanyia kazi ili kuwapatia ardhi ya kujenga viwanda,”alisema Ndikilo.
Aidha katika hatua nyingine Ndikilo amewatoa hofu kwa kuwahakikishia wawakilishi hao wa wafanyabiashara kuwa Mkoa bado una maeneo ambayo tayari yametengwa maalumu kwa ajili ya Ujenzi wa Viwanda hivyo watahakikisha wanawapa ushirikiano wa kutosha katika kila hatu ili waweze kutimiza malengo waliyojiwekea.
Katika hatua nyingine alifafanua kuwa katika eneo la Kwala kwa sasa lina Miundombinu mbinu yote Muhimu ikiwemo, Maji ya uhakika, Barabara, Umeme wa uhakika ukaribu na Bandari kavu, ukaribu wa Reli ya Mwendokasi, na ukaribu na Jiji la Dar es salaam.
Wawekezaji hao wakiongozwa na Bw. Janson Huang wameeleza kuwa wanategemea kujenga na kuanzisha viwanda zaidi ya 200 vya kuzalisha bidhaa mbali ikiwemo madawa, Kuunganishia pikiki, Viyoyozi, simu za mikononi hivyo hitaji lao la kwanza ni Ardhi ila waendelee na michakato mingine ya Uwekezaji.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment