RC KUNENGE AONGOZA MAADHIMISHO YA MEI MOSI JIJINI DAR | Tarimo Blog

 Na Humphrey Shao,Dar es Salaam.

Mkuu wa mkoa Wa Dar es Salaam,Abubakary Kunenge ameongoza mamia ya wafanyakazi wa mkoa huo katika maadhimisho ya sikukuu ya wafanyakazi (Meimosi).

Akizungumza katika maadhimisho hayo Bw.Kunenge amesema amefarijika kuona ushiriki mkubwa wa taasisi binafsi na Mashirika ya umma pamoja na serikali kuu.

"Ushiriki wenu Leo katika maadhimisho haya yakainue hali ya utendaji wenu katika maeneo yenu ya kazi kwani nimesikia risala ya tucta kwa mkoa Wa Dar es Salaam imesheheni changamoto nyingi" Amesema Kunenge.

Kwa upande wake Mmoja wa Washiriki katika Mahadhimisho hayo kutoka STAMICO, Vitusi Chanico ambaye ni afisa utumishi Amesema kuwa wafanyakazi wengi wanaonekana kuwa na Hari Sana katika Meimosi ya mwaka huu.

Ametaja kuwa wao Kama watumishi wa umma wamejipanga kuhakikisha kuwa kazi inaendelea Kama ilivyo kauli mbiu ya Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kazi Indelee.

Mkuu wa mkoa Wa Dar es Salaam,Abubakary Kunenge
Afisa Utumishi kutoka STAMICO, Vitusi Chanico akizungumza na Wahandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali
Watumishi wa Shirika la Madini nchini STAMICO Wakiwa katika picha ya Pamoja wakati wa maadhimisho ya Meimosi Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Watumishi wa Shirika la Madini nchini STAMICO Wakiwa katika maadhimisho ya Meimosi Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam wakipita mbele ya Mkuu wa Mkoa huo, Abubakary Kunenge wakati wa maandamano ya Mashirika mbalimbali
Viongozi wa Meza Kuu wakiwapungia waandamanaji wakati wa maonyesho ya vifaa.
Wafanyakazi wa Shirika la Majisafi na maji Taka la mkoa Wa Dar es Salaam DAWASA wakipita mbele ya mgeni rasmi
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2