SGT yawanoa wachimbaji wadogo Mtwara namna bora ya uchunguzi wa sampuli , uchenjuaji wa madini | Tarimo Blog

 Na Mwaandishi Wetu Mtwara

TAASISI ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) imetoa mafunzo kwa wachimbaji wadogo wa madini Mkoa wa Mtwara ambayo yamelenga kutoa mwongozo wa namna bora ya uchukuaji wa sampuli za uchunguzi na uchenjuaji wa madini.

Mafunzo hayo yalifanyika kwa siku mbili Wilayani Masasi yaliandaliwa na GST kufuatia kuwepo kwa  chanagmoto nyingi kwa wachimbaji wadogo kuhusu uchukuaji wa sampuli za uchunguzi wa kimaabara na uchenjuaji wa madini mablimbali.

Mjiolojia kutoka GST Zortosy Mpangile amesema GST alizataja changamoto hizo kuwa ni uchukuaji wa sampuli holela, wachimbaji wengi kutojua aina nzuri ya sampuli ya kupeleka maabara na sampuli wakilishi.

“Sasa baada ya kugundua hizi changamoto ambazo kimsingi zimekuwa zikiwakabili moja kwa moja wachimbaji wadogo, tukaona ni vyema na ni wakati mwafaka kuweza kuandaa haya mafunzo,” amesema.

 na kuzitaji changamoto hizo uchukuaji wa sampuli holela, wachimbaji wengi kutojua aina nzuri ya sampuli ya kupeleka maabara na sampuli wakilishi.

Akifungua mafunzo hayo, Mkuu wa Wilaya ya Masasi Seleman Mzee aliomba serikali kutuma SGT kwenda Mkoa wa Mtwara kufanya utafiti wa kina kubaini miamba mizuri kwa uchimbaji wa madini ya dhahabu katika Wilaya za Masasi na Nanyumbu ambapo yanapatikana.

Katika risala yake ya ufunguzi iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Moses Machali, Mzee amesema shughuli za uchimbaji madini ya dhahabu na madini mengi ambayo yako katika mkoa wa Mtwara hasa Wilaya za Masasi na Nanyumbu bado upo chini sana.

Kwa upande mwingine, Mkuu huyo amewataka wachimbaji wadogo walionufaika na mafunzo hayo kutumia GST katika kupata utaalamu na ujuzi katika kuongeza ufanisi katika kazi zao za uchumbaji wa madini.

Pia amewata wachimbaji hao kutumia kitabu cha mwongozo kilichoandaliwa na GST kwa namna bora ya uchukuaji sampuli za uchunguzi na uchenjuaji wa madini ambacho pia kilitumika kinatumika kutoa mafunzo hayo.

“Ni matumaini yangu kwamba kitabu hiki pamoja na mafunzo yatakayotolewa vitakuwa ni msaada mkubwa kwenu katika kuboresha utendaji kazi ili uwe wa uhakika na wenye tija,” amesema.

Kwa upande mwinginge, Katibu Mkuu wa chama cha wachimbaji Mkoa wa Mtwara, Abdallah Al Ismail ameishukuru serikali kupitia GST kuwapa mafuno hayo ambayo sasa yatawasaidia kuchimba madini bila kubahatisha.

“Mafunzo haya yatatusaidia kwa kiasi kikubwa sana, kwa sasabu sasa hivi tulikuw tunachimba bila kujua tunachimba nini, tunajaribu kutafutatafu tu, lakini kama sasa tutachimba kwa kupitia vipimo vya GST vyenye uhakiki, tutakuwa tunachimba tukiwa na uhakika tunachimba nini,” amsema.

Pia amesema mafunzo hayo yatafungua fursa nyingi kwa wachimbaji wadogo kama vile kuweza kupata mikopo kutoka kwa benki kubwa nchini kwa sababu wataaminiwa kwa kufanya uchimbaji wenye tija.

Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Moses Machali (Wa kwanza kulia) akipokea kitabu kuhusu namna bora ya uchukuaji sampuli za uchunguzi na uchenjuaji wa madini kutoka Kwa Mjiolojia kutoka Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Nchini. Kitabu hicho pia kilitumika kutoa mafunzo hayo.

Washiriki wa mafunzo ambao ni wachimbaji wadogo wa madini Mtwara wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu na waandaji wa mafunzo kutoka GST.

Mjiolojia kutoka SGT Zortosy Mpangile (aliyesimama) akitoa mafunzo Kwa wachimbaji wadogo wa madini Mkoani Mtwara kuhusu namna bora ya uchukuaji wa sampuli za uchunguzi na uchenjuaji wa madini.
Sehemu ya washiriki (wachimbaji wadogo Mtwara) wakiwa kwenye wakimsikiliza Mjiolojia (hayupo pichani) wakati wa mafunzo ya namna bora ya uchukuaji wa sampuli za uchunguzi na uchenjuaji wa madini Mkoa wa Mtwara.


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2