SHAKA AWAKUMBUSHA WANANCHI KWA UJUMLA KUENDELEA KUCHAPA KAZI, ASHIRIKI SWALA YA EID AL- FITR UJIJI MKOANI KIGOMA | Tarimo Blog

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Shaka Hamdu Shaka akizungumza na waandishi wa habari Mkoani Kigoma wakati akitoa salamu za Eid Al- Fitr za  Chama hicho kwa Watanzania.
Shaka Hamdu Shaka ambaye ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM( kushoto) akiteta jambo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Selemani Jafo baada ya kuungana na waislamu wa Mkoa wa Kigoma kuswali swala ya Eid Al- Fitr.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Shaka Hamdu Shaka akishiriki kwenye Ibada ya swala ya Eid Al - Fitr akiwa Ujiji mkoani Kigoma.

Na Mwandishi Wetu

KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi( CCM) Shaka Hamdu Shaka amewahimiza wananchi wote kwa ujumla kufanya kazi kwa bidii ili kuweza kuzalisha ili kujiletea maendeleo na kukuza uchumi wa Taifa, sambamba na kutimiza kutunza na kuimarisha hali ya amani, utulivu, umoja na Mshikamano katika nchi yetu.

Amesema hayo leo baada ya kumalizika kwa swala ya Eid  Al- Fitr mbapo Shaka aliungana na  waumini wa Dini ya Kiislam Mkoa wa Kigoma kushiriki swala hiyo iliyosaliwa katika Uwanja wa Stendi Mpya ya Ujiji-Kigoma mapema leo tarehe 14 Mei 2021.

Swala hiyo iliyoongozwa na Sheikh wa Mkoa wa Kigoma Sheikh Hassan Kiburwa ilihudhuriwa pia na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wa zalendo Ndugu Juma Duni Hajji, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Ndugu Suleiman Jafo.

Pia, Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini  Kilumbe Shaban Ng'enda,  Mbunge wa Sumbawanga mjini Ndugu Aeshi Hillary na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma Ndugu Maryam Ditopile. 

Katika salamu zake za Eid Al-Fitr kwa waumini wakati wa Swala, Mwenezi Shaka amefikisha salamu za Eid kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Samia Suluhu Hassan, ambapo amewaambia waumini kuwa;

"Mwenyekiti wetu na Rais wenu mpendwa amenituma niwaeleze kuwa anawapenda na anawatakia heri na furaha katika siku muhimu  duniani"

Amewaomba waumini kuliombea Taifa pamoja na kumuomba MwenyeziMungu amjaalie Mwenyekiti wa CCM na Rais wetu Ndugu Samia Suluhu Hassan, ampe Afya njema, maono na msimamo thabiti katika kuiongoza nchi yetu.

Aidha amesisitiza kuhusu umuhimu wa wananchi wote kufanya kazi kwa bidii ili tuweze kuzalisha ili kujiletea maendeleo na kukuza uchumi wa Taifa, sambamba na kutimiza kutunza na kuimarisha hali ya amani, utulivu, umoja na Mshikamano katika nchi yetu.


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2