Wanufaika wa Tasaf wafuga samaki kwa ajili ya kitoweo na kukuza kipato | Tarimo Blog

 

Na Amiri Kilagalila,Njombe

 

Ili kukabiliana na hali ya udumavu kwa watoto mkoani Njombe,wananchi wanaonufaika na mradi wa kunusuru kaya masikini (TASAF) kata ya Kidugala wilayani wanging'ombe wamelazimika kuanzisha mradi wa ufugaji wa samaki kwa ajili ya kubadili mlo na kukuza kipato.

 

Kitakwimu mkoa wa Njombe unashika nafasi ya pili nchini kwa kuwa na asilimia  49.6 za utapiamlo na udumavu,ambapo kutokana na uwepo wa changamoto hiyo baadhi ya kaya masikini wilayani wanging”ombe wameamua kuanzisha mradi wa ufugaji samaki ili kuwanusuru watoto wenye umri chini ya miaka mitano.

 

Baadhi ya wakazi hao  kutoka kidugala akiwemo Atu  Ng'ahala na Balton Kizumbe wameanzisha mradi huo ambao umekuwa na manufaa makubwa kwao na watoto wao.

 

“Tunaufurahia huu mradi kwasababu ni sehemu ya kitoweo kulingana na afya zetu za watu wa mkoa wa Njombe kwa hiyo tunawashukuru sana Tasaf kwasabu mrai umekuwa ni chachu hata kwa wengine”alisema Balton Kizumbe

 

Kutokana na uwepo wa tatizo la utapiamlo na udumavu kuathiri ndani ya kata ya Kidugala wilayani Wanging’ombe,diwani wa kata hiyo bwana Wilson Mbilinyi  amesema katika lishe bora samaki ni muhimu kwa afya za watoto .

 

“Tuko sasa kwenye jitihada za kuhakikisha tunazalisha samaki kwa wingi ili tuweze kupambana na hili tatizo la udumavu “Wilson Mbilinyi 

 

Bertha Nyigu ni Afisa lishe  mkoa wa Njombe  ambaye amesema maono ya wakazi wa mkoa wa Njombe kwa sasa ni kuona wanakuwa na watu wenye lishe bora hususani watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano.

 

“Mikakati imewekwa katika mambo makubwa ili kupunguza udumavu ikiemo.kupunguza kiwango cha udumavu kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano”alisema Betha Nyigu

 Mradi wa kunusuru kaya masikini tasaf hapa nchini umekuwa ukitoa fedha taslimu kwa walengwa ambazo zimekuwa zikiwasaidia kujikimu kwa kuanzisha miradi midogo midogo inayowasaidia katika kuendesha familia na hata kuongeza kipato.


 
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2