WATAALAMU WAELEKEZI WA MIRADI WATAKIWA KUFANYA UFUATILIA WA TATHIMINI KUBAINI KAMA KUNA UFANISI AU CHANGAMOTO | Tarimo Blog

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mohammed Khamis Abdullah amewataka wataalamu waelekezi wa miradi kufanya ufuatiliaji wa tathmini ili kubaini kama kuna ufanisi au changamoto ili waweze kuzitatua.

Abdullah ametoa kauli hiyo leo wakati akifungua Mafunzo ya Mifumo ya Ufuatiliaji na Tathmini, Uhasibu na Ugavi kwa wataalamu wawezeshaji wa halmashauri za wilaya zinazotekeleza Mradi wa Kurejesha Ardhi iliyoharibika na kuongeza Usalama wa Chakula katika maeneo kame nchini (LDFS) mjini Singida.

Alisema hata kama fedha za mradi zikisimamiwa vizuri na wahasibu, na manunuzi ya vifaa na huduma yakasimamiwa vizuri na maafisa, manunuzi bado ni muhimu kufanyike ufuatiliaji na tathmini katika utekelezaji wa shughuli za mradi.

“Kazi ya ufuatiliaji na tathmini ni muhimu sana katika utekelezaji wa mradi wowote. Sehemu hii ndiyo yenye kubainisha viashiria muhimu vya mradi iwapo utekelezaji wa mradi unakwenda vizuri au la na kusaidia kubaini changamoto za utekelezaji wake mapema ili kuweza kuzifanya marekebisho yanayohitajika, hivyo, ni muhimu kazi ya ufuatiliaji na tathmini nayo ifanyike kwa weledi ili thamani ya fedha (value for money) iweze kuonekana,” alisema.

Aidha, Naibu Katibu Mkuu huyo aliwakumbusha washiriki hao kuwa ufanisi na matokeo chanya ya mradi huu hayawezi kupatikana iwapo hakutakuwa na usimamizi madhubuti wa fedha na hivyo utekelezaji unaweza usifanyike kwa viwango vinavyotakiwa.

Aliongeza kuwa uhasibu ni kada muhimu katika usimamizi wa fedha za mradi ambao watasaidia katika kushauri na kusimamia namna sahihi ya matumizi ya fedha za mradi hivyo mafunzo hayo yatawasadia kupata maarifa yatakayowawezesha kusimamia fedha vizuri ili kufikia malengo yaliyokusudiwa katika utekelezaji wa mradi.

Kwa upande wake Mratibu wa Mradi wa LDFS Joseph Kihaule alisema mradi huo ulioanza kutekelezwa mwaka 2017 umelenga kuangalia mabadiliko ya tabianchi yanaathiri vipi uzalishaji hasa katika maeneo kame.

Pai alisema mradi utasaidia kuboresha mifumo ikolojia ya kilimo ambayo itawezesha kuongeza uzalishaji wa chakula na kuchangia kuboresha mazingira katika Halmashauri za wilaya husika.

Sambamba na hilo mratibu huyo alibainisha kuwa kupitia mradi huo kutakuwa na usimamizi endelevu wa mifumo ikolojia inayochangia kutoa huduma muhimu za uzalishaji kwenye maeneo ya ardhi, maji, misitu, bioanuai kwa madhumuni ya kuboresha uzalishaji.

“Mradi unategemea kuongoa hekari 9,000 kati ya hizo hekari 3,000 zitumike kwa kilimo hifadhi na rafiki wa mazingira na usimamizi endelevu wa ardhi; hekari 4,000 za ardhi zilizo haribika zitaongolewa na kutumika katika kuboresha nyanda za malisho; 2,000 nazo zitatumika kwa ajili ya hifadhi ya bionuai na misitu,” alisema Kihaule.



Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Mohammed Khamis Abdullah akifungua Mafunzo ya Mifumo ya Ufuatiliaji na Tathmini, Uhasibu na Ugavi kwa wataalamu wawezeshaji wa halmashauri za wilaya zinazotekeleza Mradi wa Kurejesha Ardhi iliyoharibika na kuongeza Usalama wa Chakula katika maeneo kame nchini (LDFS), yaliyoanza leo Mei 3 na yatamalizika Mei 7, 2021 mjini Singida.

 


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2