'WATU WAPATE HUDUMA HOSPITALINI PF3 ITAFUATA...WATU WANAPOTEZA MAISHA' | Tarimo Blog

 

Na Said Mwishehe, Michuzi TV

RAIS Samia Suluhu Hassan amesema kuna haja ya kutazamwa upya kwa sheria ambayo inaelekeza mtu yoyote anayepata ajali lazima awe na PF 3 ya Jeshi la Polisi kwani inasababisha watu kufa kwa kukosa matibabu licha kufikishwa hospitalini.

Akizungumza leo viongozi wa ngazi mbalimbali wakiwemo maofisa wa Jeshi la Polisi nchini, Rais Samia amesema watu wanaopata ajali wanaumia kwa viwango tofauti tofauti , mwingine anapoumia akifika hospitali inabidi apate matibabu haraka haraka lakini sheria yetu ni  kwamba hawezi kuhudumiwa mpaka iende PF3.

"Watu wanafia pale hospitali , watu wanapomchukua mtu aliyepata ajali wanaumuokota ni kupaniki mbio hospitali hawakumbuki kwanza kurudi Polisi , kwa hiyo niombe sana hii sheria muiangalie, mtu anapofikishwa hosptitali apate huduma mambo mengine ya kipolisi yaendelee.Tunapoteza watu kwasababu ya kipengele kidogo cha PF3,"amesema Rais Samia.

Katika hatua nyingine, Rais Samia ametumia nafasi kueleza kwamba vitendo vya udhalilishaji bado vinaendelea  kushamiri kwa mfano  wamemsikia Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Simon Sirro akieleza vitendo vya udhalilishaji vimeendelea kuongezeka.

"Januari hadi Apiliri mwaka 2020 vitendo vya udhalilishaji vilikuwa 398  na kipindi hiko hiko kwa mwaka huu vimefikia 458 , kwa hiyo kuna ongezeko la vitendo hivyo na hapa nitoe mwito kwa jamii, kuweka mkazo zaidi kwenye malezi na vitendo hivi vinatokea ndani ya familia zetu.

"Na vinapogusa familia au ukoo mambo yale yanafichwa fichwa na kama yanafichwa watendaji wataendelea kutenda wakijua yatazungumzwa na kutozwa faini kifamilia na yataishia hapo. Niombe sana jamii ya kitanzania kujitokeza sasa kufuata vombo vya sharia ili tusaidiane , tuchangie wote pamoja kwenye kukomesha vitendo hivi."


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2