WAZIRI BITEKO AWAHAKIKISHIA WAUZAJI WAKUBWA WA MADINI SERIKALI KUENDELEA KUISIMAMIA SEKTA HIYO ILI IWE NA TIJA | Tarimo Blog

Na Said Mwishehe,Michuzi TV

WIZARA ya Madini imesema itaendelea kuisimamia sekta ya madini ili iendelee kuwa na tija kwa wananchi wote hasa kwa kuzingatia sekta hiyo imekuwa na mchango mkubwa katika ukuaji uchumi wa Taifa la Tanzania.

Akizungumza leo Mei 12,2021 wakati akifungua mkutano wa wauzaji wakubwa wa madini uliofanyika Dar es Salaam, Waziri wa Madini Dotto Biteko amesisitiza sekta ya madini inamchango mkubwa wa ukuaji uchumi.Mkutano huo umeshirikisha pia watalaamu kutoka Mamlaka za Serikali zinazosimamia sekta hiyo.

"Serikali inaendelea kusimamia sekta ya madini ili iendelee kuwa na tija kutokana na sekta hhii kuongoza kwa ukuaji wa uchumi wa asilimia saba kutoka asilimia 3.8 ya mwaka 2015, na kutajwa kuongoza kwa kuliingizia Taifa pato la kigeni,"amesema Biteko na kuongeza asilimia 52.4 ya bidhaa za Tanzania zinazouzwa nje ya nchi zinatokana na mazao ya madini.

Hivyo kuifanya sekta hiyo izidi kuimarika kwenye mapato na kuchangia sekta nyingine katika ukuaji wa uchumi huku akisisitiza kupitia kikao hicho cha leo yote ambayo yatazungumzwa na kupendezwa na wauzaji hao wakubwa wa madini nchini Wizara yake itayafanyia kazi.

Kwa kufanya majadiliano lakini ameweka wazi kuna baadhi ya mambo hatarudi nyuma lazima waendelee kuyasimamia. "Sekta ya Madini imetoka mbali, imepita katika historia ndefu sana.

"Imetoka kwenye kundi ambalo biashara ilikuwa ikifanywa kwa kificho, leo imekuwa ni sekta ambayo biashara inafanywa kwa uwazi, mchango wake unaweza kupimwa katika maeneo mbalimbali ikiwepo kukuza uchumi wa nchi kutoka asilimia 3.8 hadi asilimia saba.



"Kikubwa ambacho tunaendelea kukihamasisha ni kwamba madini yaliyopo nchini yananufasha wananchi wote na tumekuwa tukiitoa rai kwa jamii kutokuwa na mawazo hasi dhidi ya kampuni za madini.Tunaendelea kuhamasisha ushirikiano kati ya kampuni za migodi ya madini na wananchi katika mazingira yanayozunguka,"amesema Waziri Biteko.

Aidha Biteko amesema Wizara ya Madini itayafanyia kazi mapendekezo sita yaliyotolewa na wachimbaji na wauzaji wakubwa na wa kati wa madini wakati wa kikao hicho.

Baadh ya mapendekezo hayo ni kuweka vivutio na sera nzuri za biashara ya madini ili kuwavuta wawekezaji wengi zaidi wa ndani na nje ya nchi, kufanya tafiti za madini, kuweka mazingira wezeshi ya biashara hiyo, kuwa na ulinzi na usalama wa uhakika wa biashara hiyo, uibuaji wa vipaji na mafundi wa madini wa kitanzania na uboreshwaji wa mindombinu kwenye maeneo ya migodi.

Awali Mwenyekiti wa Chemba ya Madini Mhandisi Philbert Rweyemamu amesema pamoja na mambo mengine kuna haja wadau hao wa madini kujadiliana na kuangalia namna bora ya kuongeza migodi mipya ya uchimbaji wa madini na kuongeza mitaji kutoka katika masoko ya hisa ya nchi za nje.

Ameongeza wanahitaji fedha za wawekezaji kutoka nje ya nchi kwani soko la hisa la Dar es Salaam halijakidhi mahitaji ya sasa na mara nyingi fedha za kuanzisha hiyo miradi zinatoka kwenye masoko makubwa ya hisa ya nchi za nje.

"Kwa hiyo tunashauri Wizara tujadiliane kwa yale ambayo tunafikiri kama yakiwekewa mkazo au yakabadilishwa, yataongeza tija na tutaona migodi mipya ikianzishwa,"amefafanua.


Waziri wa Madini Dotto Biteko akizungumza leo Mei 12,2021 wakati akifungua kikao cha wauzaji na wachimbaji wakubwa madini ambao wamekutana kwa lengo la kuweka mikakati itakayosaidia sekta hiyo kuwa na tija.


Mwenyekiti wa Chemba ya Madini Mhandisi Philbert Rweyemamu akifafanua jambo wakati wa kikao kati ya wauzaji na wachimbaji wakubwa wa madini na Waziri wa Madini Dotto Biteko .Kikao hicho kimefanyika leo Mei 12,2021 jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya wauzaji na wachimbaji wakubwa wa madini wakiwa kwenye kikao kati yao na Waziri wa Madini Dotto Biteko(hayupo pichani) ambapo wamekutana kujadili masuala mbalimbali yanayohusu sekta hiyo.

Baadhi ya wachimbaji wakubwa wa madini wakiandika baadhi ya maelezo kutoka Waziri wa Madini Dotto Biteko aliyekuwa akizungumza na wachimbaji hao leo Mei 12,2021 jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Said Mwishehe)

Sehemu ya washiriki wa kikao cha wauzaji na wachimbaji wakubwa wa madini wakijadiliana jambo wakati kikao hicho.

Baadhi ya wauzaji na wachimbaji madini kutoka kampuni mbalimbali wakimsikiliza Waziri wa Madini Dotto Biteko(hayuko pichani).


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2