Waziri wa Madini Doto Biteko amewataka wachimbaji wadogo wa madini mkoani Geita kutumia taarifa za kitaalam za jiosayansi pamoja na kuitumia Maabara ya Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) katika shughuli zao za uchimbaji Madini nchini.
Biteko amesema hayo wakati wa ufunguzi WA mafunzo kwa wachimbaji wadogo yanayohusu Namna Bora ya Uchukuaji wa Sampuli za Uchunguzi na Uchenjuaji wa Madini Tanzania yanayotolewa na (GST).
Akiitimisha hotuba ya kufungua mafunzo hayo Biteko aliwasisitiza wachimbaji wadogo kutumia fursa ya mafunzo hayo ya nadharia na vitendo ili kuleta tija zaidi na kufanya uchimbaji wa uhakika bila kupoteza muda na mitaji pamoja na kuzuia uharibifu wa mazingira.
Mafunzo haya yanatolewa katika mikoa tisa nchini.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment