Akizungumza wakati wa kuadhimisha siku ya wafanyakazi duniani, ambapo WLAC wameadhimisha katika viwanja vya mapilau eneo la Mwananyamala Mkoani Dar es Salaam,
Mwanasheria kutoka kituo hicho Consolata Chikoti, amesema wanawake na vijana ndio kundi kubwa ambalo limekuwa likiangukia katika ajira zisizo rasmi na hivyo mara nyingi kujikuta wakikosa kazi.
"Sisi kama kituo cha msaada kwa wanawake WLAC ambao tunatekeleza Mradi wa kuwawezesha wanawake na vijana katika masuala ya sheria na ajira, tunatoa wito kwa Serikali kujitahidi kuhakikisha wanatengeneza ajira nyingi zaidi ili kuweza kuwaingiza wakina mama na vijana katikati sekta maalumu kwa maslahi mazuri ili waweze kuwa na ulinzi wa kijamii katika masuala ya ajira," amesema Chikoti.
“Kaulimbiu ya siku wafanyakazi mwaka huu inasema ‘maslahi bora, mshahara juu, kazi iendelee’.
Katika sherehe za mwaka huu za wafanyakazi, WLAC tumeamua kukutanisha kundi hili la wafanyakazi waliokwenye sekta isiyo rasmi ili na wao wajione kama wenzao na pia tutumie fursa hii kuwapa elimu ya kutambua haki zao mbalimbali na namna ya kuzipigania.
Amesema, pamoja na kwamba Serikali imeonyesha nia nzuri katika kusimamia maslahi ya wafanyakazi nchini hususani kupitia kaulimbiu hii ya mwaka huu lakini bado kuna kundi ambalo mara nyingi limekuwa likisahaulika, kundi hilo ni la watu waliopo katika sekta ya ajira isiyo rasmi, ambalo lina watu wengi wakiwemo wanawake na vijana. "Kundi hili lina watu ambao wanafanya kazi kwa bidii sana lakini ajira zao hazina ulinzi.” ameongeza Chikoti.
Aidha ameongeza kuwa kumekuwa na ukosefu wa ajira, hususani kwa wanawanawake na vijana ambapo wengi wanamaliza vyuo wanavyeti na wanaujuzi lakini kumekuwa na nafasi chache za kuajiriwa katika mfumo rasmi hivyo wengi wanajikuta katika mfumo usio rasmi na wengine kujiajiri.
“Wengi wao wanafanya kazi katika viwanda, wengine wanaajiriwa kama wapishi, wafanya usafi, wadada wa kazi kwenye majumba, kwa ujumla wao hili ni kundi muhimu sana ambalo linaonekana kusahaulika sana, lakini ni vema kwa sababu nalo linafanya kazi kama walivyo wafanyakazi wengine, wakapewa kipaumbele na wao hususani kwa kutengeneza sera na sheria ambazo zitalinda ajira zao.”
Chikoti amebainisha kuwa, WLAC kama kituo cha wanasheria wabobezi, wamekuwa wakikupambana na idadi kubwa ya wafanyakazi wasio na ajira rasmi wakilalamikia kunyanyaswa na kutokutendewa haki na waajiri wao kama ilivyo kwa wafanyakazi wengine.
Naye Diwani wa Kata ya Makumbusho, Mohammed Ally, amesema changamoto ya kutokuzingatiwa haki za wafanyakazi katika sekta isiyo rasmi limekuwa ni la muda mrefu na kwamba kuna haja ya kutafutiwa ufumbuzi.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment