WLAC WASHEHEREKEA SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI KWA KUTOA ELIMU TANDIKA | Tarimo Blog

WAFANYAKAZI wa Kituo cha Msaada wa Kisheria kwa Wanawake (WLAC) washeherekea siku ya wafanyakazi kwa kutoa elimu  kwa wananchi wa kata ya Tandika Mtaa wa Nyambwera Mkoa wa Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa kutoa elimu kwa wananchi wa mtaa wa Nyambwera, Afisa Sheria kutoka Kituo cha Msaada wa Kisheria kwa Wanawake (WLAC), Barcoal Deogratius leo Mei Mosi, 2021 amesema kuwa lengo la kutoa Elimu kwa wananchi hao ni kutaka sheria ya ajira iweze kuenea kila mahali ili kila mwananchi aweze kujua wajibu wao.

"Siku ya leo tunaadhimisha simu ya wafanyakazi duniani WLAC tumekuja kata hii ya Tandika mtaa wa Nyambwera kutoa elimu ya sheria ya mahala pa kazi kwa wafanyakazi wa ndani pamoja na wafanyakazi wa sekta zisizo rasmi na sekta rasmi." Amesema Deogratius

Amesema kuwa katika kumalizia muda wa miaka miwili wa Mradi wa uwezeshaji wa jamii kisheria juu ya sheria na haki mahala pa kazi unaofadhiliwa na shirika la Legal Services Facility wanaendelea kutoa elimu kwa wananchi mitaani kupitia ofisi za Serikali za mtaa yao.

"Leo kumekuwa na mwitikio mkubwa wa wananchi licha ya kuwa na hali ya hewa ya Mvua katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Dar es Salaam wananchi wamekuja kutusikiliza na kujua ni nini tunawafundisha juu ya Masuala ya Sheria na haki mahala pa kazi." Amesema Deogratius

Hata hivyo Deogratius amesema wananchi wanatakiwa kujua haki zao mahala pa kazi haijarishi upo katika sekta rasmi ama sekta isiyo rasmi.

Kwa upande wake mwananchi wa Mtaa wa Nyambwera, Mwanaid Salum amesema kuwa ametambua baadhi ya sheria ya ajira na atachukua kama faida kwake na kuwafundisha watu wengine wanaowanyanyasa wafanyakazi.

Nae Mkazi wa Mtaa wa Nyambwera, Idd Ramadhan ameowaomba wafanyakazi wa Kituo cha Msaada wa Kisheria (WLAC) kuandaa mafunzo mengine ili wananchi waweze kuelewa zaidi haki zao.

Wafanyakazi wote wa sekta rasmi na sekta zisizo rasmi wanahaki sawa kwani sheria mama ni moja tuu inayoongoza katika masuala  mazima ya haki na usawa mahala pa kazi nayo lazima ifuatwe." Amesema Deogratius

Licha ya hayo katika kipindi cha Maswali na majibu wananchi wameweza kuuliza maswali ya sheria ya ardhi, sheria za ndoa pamoja na sheria za Mirathi kwa wanafamilia.
Afisa Sheria kutoka Kituo cha Msaada wa Kisheria kwa wanawake, Rodger Michael akizungumza leo na wananchi wa kata ya Tandika mtaa wa Nyambwera walipofika WLAC kutoa elimu ikiwa ni njia mojawapo ya kusheherekea siku ya wafanyakazi duniani ambayo hufanyika kila mwaka.

Mwananchi wa Mtaa wa  Nyambwera akizungumza katika uhamasishaji wa kuijua sheria na haki kwa wafanyakazi wa sekta rasmi na sekta zisizo rasmi ngazi ya jamii akizungumza na wananchi wa mtaa wa Nyambwera leo Mkoani Dar es Salaam.

Kushoto ni mmoja ya wahamasishaji wa kuijua sheria na haki kwa wafanyakazi wa sekta rasmi na sekta zisizo rasmi ngazi ya jamii akizungumza na wananchi wa mtaa wa Nyambwera leo Mkoani Dar es Salaam.

 Moja ya wahamasishaji wa kuijua sheria na haki kwa wafanyakazi wa sekta rasmi na sekta zisizo rasmi ngazi ya jamii akizungumza na wananchi wa mtaa wa Nyambwera leo Mkoani Dar es Salaam.


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2