Na Woinde Shizza , Michuzi Tv Arusha
ZAIDI ya hekari laki tatu na nusu za miti zinapotea kwa mwaka kutokana na ukatiji miti unaofanyika mara kwa mara.
Aidha pia watanzania wametakiwa kujenga tabia ya kupanda miti ya matunda kwa wingi katika maeneo yao kwani inafaida nyingi katika afya ya binadamu pamoja na utunzaji wa mazingira.
Hayo yamebainishwa na meneja mkuu wa miradi kutoka asasi ya kilele inayojishughulisha na kilimo cha horticulture yaani mboga, matunda na mimea itokanayo na mizizi pamoja na viungo(TAHA) Antoni Chamanga alipokuwa anaongea na waandishi wa habari wakati wakikabidhi miti ya matunda 274 Katika shule ya msingi Kimandafu iliopo wilayani Arumeru mkoani Arusha.
Alisema kuwa ni vyema watanzania wakajijengea tabia ya kupanda miti katika maeneo yao kwani inafaida nyingi katika maisha ya binadamu ikiwemo kulinda mazingira, ni lishe bora kwani ukila tunda unaboresha afya yako pia unaongeza kipato kwa yule anaehusika na upandaji wa miti hiyo.
"Kila mwaka tumekuwa tunapoteza miti mingi kutokana na ukataji miti unaofanywa mara kwa mara lakini iwapo tukipanda miti ya matunda kama mapera, maembe na mengineyo itatusaidia kupunguza tatizo hilo kwani ,miti hiyo aitakatwa tena kwakuwa itakuwa inazaa matunda ambayo kila mtu atakula."Alisema Chamanga
Alisema miti hii ya matunda wameitoa wao wakishirikiana na washirika wao wenza ambao ni Trias na kubainisha kuwa zoezi hili niendelevu na wameanza na shule za wilayani Arumeru na wanatarajia kupeleka miti hii katika maeneo mbalimbali hapa nchini kwa kipindi cha miaka mitano ,na wanaamini miti hii itasaidia kulinda ,kutunza kuboresha hali ya hewa pamoja na mazingira kwa ujumla.
Kwa upande wake meneja miradi kutoka Trias Lillian Makoy alisema kuwa wameanza kufanya kazi na Taha mwaka 2017 na wanatekeleza mradi unaojulikana kwa jina la strong ,mradi unaohamasisha kurudisha misitu iliopotea ambapo alisema mradi huu unatekelezwa Katika mkoa wa Arusha pamoja Zanzibar na mradi huu itasaidia wanafunzi kupata matunda katika shule zao.
Alisema zoezi hili litasaidia kupunguza athari zinazotokana na mabadiliko ya hali ya hewa na mazingira pia swala hili la upandaji miti ni endelevu na mtambuka.
Akitoa shukrani mara baada ya kupokea miti hiyo ya matunda mkuu wa shule ya msingi Kimandafu, Hellen Tundie aliishukuru Taha kuwa kuwapatia miti hiyo ya matunda na kubainisha kuwa itawasaidia kutunza mazingira pamoja na kuwapa lishe bora wanafunzi wanaosoma hapo shuleni.
Aidha alisema kuwa elimu walioipata ya upandaji miti itawasaidia wao na wanafunzi waliopo apo shuleni kuweza kupanda miti katika ubora ambapo pia itawasaidia hata wanafunzi kuendeleza elimu hii kwa wengine kule mtaani.
Meneja mkuu wa miradi kutoka asasi ya kilele inayojishughulisha na kilimo cha horticulture yaani mboga, matunda na mimea itokanayo na mizizi pamoja na viungo(TAHA) Antoni Chamanga akiongea na waandishi wa habari wakati wakikabidhi miti ya matunda 274 Katika shule ya msingi Kimandafu iliopo wilayani Arumeru mkoani Arusha. Afisa lishe wa asasi ya kilele inayojishughulisha na kilimo cha horticulture yaani mboga, matunda na mimea itokanayo na mizizi pamoja na viungo(TAHA)Rosalia Aloyce akiwapa elimu ya lishe wanafunzi wa shule ya msingi Chemi chemi iliopo wilayani Arumeru mkoani Arusha juzi alopotembelea shule hiyo kwa ajili ya kuwapa elimu ya lishe.
(Picha na Woinde Shizza, ARUSHA)
Mkuu wa idara ya uzalishaji kutoka Asasi ya kilele inayojishughulisha na kilimo cha Horticulture yaani mboga, matunda na mimea itokanayo na mizizi pamoja na viungo(TAHA) akiwawlekeza wanafunzi wa shule ya msingi Kimandafu namna ya kupanda Miti ya matunda iliyotolewa kwa shule hiyo na TAHA pamoja na washirika wao Trias.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment