BENKI YA AKIBA YASHIRIKI ZOEZI LA KUTOA NA KUCHANGIA DAMU | Tarimo Blog


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam 

Kama sehemu ya jamii pamoja na kutambua umuhimu wa kuokoa maisha, Benki ya Akiba imeshiriki kikamilifu katika zoezi muhimu la kuchangia damu ikiwa ni sehemu ya siku ya maadhimisho ya siku ya kuchangia damu ambapo kilele cha maadhimisho yake ni June 14, 2021.

Akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa zoezi hilo, Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano, Benki ya Akiba, Dora Saria amesema jumla ya wafanyakazi takribani 30 kutoka Benki hiyo wamejitolea kushiriki katika zoezi la kuchangia damu kutokana na umuhimu wa zoezi husika, ili kuunga mkono jamii.

“Benki ya Akiba imekuwa  mshiriki mahiri katika masuala ya kijamii kwa kutoa misaada katika sekta za Elimu, Mazingira na Afya kama ambavyo siku ya leo tumeshiriki katika zoezi hili kuchangia damu”, amesema Dora.

Pia kwa niaba ya Benki hiyo, Dora amesema wanatoa rai kwa Taasisi nyingine mbalimbali na Watanzania wote kwa ujumla kushiriki katika zoezi hilo kwa ajili ya kuokoa maisha ya Watanzania wenye uhitaji wa damu.

Wananchi wakiendelea na Zoezi la kuchangia damu likiendelea jijini Dar es Saalam kuelekea kilele cha maadhimisho June 14, 2021.
Mmoja wa Wafanyakazi wa Benki ya Akiba akipima kabla ya kuanza zoezi la kuchangia damu lilofanyika jijini Dar es Salaam ikiwa ni maandalizi kuelekea maadhimisho yake June 14, 2021.




Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2