BENKI YA DUNIA YAPONGEZWA KWA MISAADA IKIWEMO MIKOPO NA RUZUKU INAYOIPATIA ZANZIBAR | Tarimo Blog

 Waziri wa Nchi Afisi ya Rais, Fedha na Mipango,Mhe. Jamal Kassim Ali, leo amekutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia (WB) kanda ya Afrika group 1, Dk. Taufila Nyamadzabo, ofisini kwake Vuga. Mhe. Jamal ameipongeza Benki hiyo kwa misaada ikiwemo mikopo na ruzuku mikopo inayoipatia Zanzibar kwani imechangia kuimarisha ustawi bora na maendeleo Nchini.

Mhe. Jamal amesema miradi mikubwa miwili nayo ni BIG-Z imetengewa Dola Milioni 150 na ZESTA imetengewa Dola Milioni 142, Miradi hiyo iliyoidhinishwa na Benki ya Dunia itaanza hivi karibuni na itachochea kwa kasi kubwa ukuwaji wa Uchumi Pamoja na maendeleo ya Zanzibar na watu wake.

kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia (WB) kanda ya Afrika Group 1 dkt. Taufila Nyamadzabo, amesema Benki ya Dunia itasaidia Zanzibar katika miradi mbali mbali ya kimkakati ikiwemo eneo la Uchumi wa Buluu.

Pia Dkt. Taufila Nyamadzabo, amesema Benki ya Dunia iko tayari  kusaidia ushiriki wa sekta binafsi katika Maendeleo. Aidha dkt. Taufila amesema kuwa sekta ya elimu na Afya ni sekta muhimu katika Maendeleo hivyo wako tayari kushirikiana na Serikali iweze kufikia malengo iliyojiwekea.



 


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2