Mtendaji wa kijiji apandishwa kizimbani kwa kutishia kuua | Tarimo Blog

Na Amiri Kilagalila,Njombe

Kesi namba 159 ya mwaka 2021 inayohusu jinai kwa mara ya kwanza imesomwa katika mahakama ya mwanzo mjini Njombe ikimuhusisha mtendaji wa kijiji cha Lilombwi kata ya Kifanya mkoani Njombe kwa kosa la kutishia kuua kwa maneno chini ya kifungu namba 89 kifungu kidogo cha pili B sura ya 16 marejeo ya mwaka 2016.

Akisoma mashitaka dhidi ya mshitakiwa Pascal Mkombwe mwenye umri wa miaka 52, hakimu mkazi wa mahakama ya mwanzo mjini Njombe, mheshimiwa Barnaba Muangi amesema kwa mujibu wa hati ya mashitaka iliyowasilishwa katika mahakama hiyo ni kuwa mnamo tarehe 4 mwezi Mei mwaka 2021 majira ya saa mbili usiku huko katika Kijiji cha Lilombwi kata ya Kifanya, mshitakiwa Pascal Mkombwe alimtishia kwa maneno Bwana Thadei Nichombe wote wakazi wa Kifanya kuwa hayupo tayari kumuona mwanae anapotea kwa kesi ya mashamba huku akijua kufanya hivyo ni kosa kinyume na sheria za nchi.

Hata hivyo mshitakiwa huyo amekana kutenda kosa hilo,ambapo amedhaminiwa na Mwenyekiti wa kijiji cha Lilombwi kwa bondi ya shilingi laki tano kwa mujibu wa sheria na yupo nje kwa dhamana hadi tarehe 15 Juni, mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.


 

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2