FILAMU 15 ZA TANZANIA ZAPETA TAMASHA LA ZIFF2021 | Tarimo Blog

 



Mkurugenzi wa ZIFF 2021, Profesa Martin Mhando akizungumza na Waandishi wa Habari  (hawapo pichani) wakati wa kutangaza filamu 65 zilizochaguliwa ambazo zitakazoonyeshwa Visiwani humo kunzia 21-25 Mwaka huu, Ngome kongwe, Zanzibar.


-Filamu 65 kuonyeshwa kwa siku tano Unguja

Na Andrew Chale, Zanzibar

FILAMU 15 za Watanzania zimefanikiwa kupenya kwenye kinyang'anyiro cha mchujo wa filamu zaidi ya 240 zilizowasilishwa kwenye Tamasha la 24 la Filamu la Kimataifa la Nchi za Majahazi [ZIFF], ambalo litafanyika kuanzia Julai 21-25 mwaka huu mjini Unguja, Zanzibar.

Akizungumza wakati wa kutangaza rasmi filamu zilizochaguliwa mwaka huu, Mkurugenzi wa ZIFF 2021, Profesa Martin Mhando  alisema zaidi ya filamu 240  kutoka nchi mbalimbali duniani zilizotuma, Jopo wamefanikiwa kuchagua filamu 65 bora zaidi huku kati ya hizo filamu 15  ni za kutoka Tanzania.

"Nchi zaidi ya 25, ikiwemo Taifa la Estonia wameweza kutuma filamu yao. Kwa uwakilishi wa Tanzania mwaka huu wamejitahidi na umezidi kuliko miaka yote ya nyuma ya ZIFF.  

Filamu 15 pekee zimetoka Tanzania huku Kenya ikitoa filamu 10, Uganda filamu 5 na kwa Afrika Kusini wao wametoa filamu." Alisema Prof. Mhando.

Ameongeza kuwa, filamu hizo 65 zilizochaguliwa, kuna  filamu ndefu 11, filamu za Makala 11 na filamu fupi na karagosi 40.

Prof. Mhando amezitaja filamu za Tanzania ni pamoja na; Binti, Decision, Dream, Murasi, Neema, Nyara, Salama, Shujaa wetu, Simba, Timela, Usiku mrefu, Nyundo, Kijiji changu huku  kwa Animation ama katuni ni Mbuland na Mozizi.

Filamu zingine ni pamoja na; A fool God, A trip of Heaven, Adam, Al sit, Carton rouge, Catch out, Coffee place, Days of Cannibalism, Deliveries, Bablinga, Bottleneck, Breaking ground, Dream child, Banyalga, Dreams of trains, Excuse, Fakh (The Trap), Heart attack, If Objects could talk na Interstate 8.

Pia zipo Itswa, Joy’s Garden, Letter to my child, Mission to rescue, Morning after, My culture my music, Naisula, Njaa, Nursery rhymes, Revolution, Shaina, Sikelela tapes, Softie, Sororal, Tales of the Accidental city, Tazara stories, The blind date, The Colonels stray, The fever, The Grandpa, The Handyaman, The Heartbeat, The Letter, To Zanzibar, Underestimated Villain, Walled Citizen na Why U hate.

Aidha, Prof. Mhando amesema kuwa, mwitiko wa filamu mwaka huu umeshuka kidogo kutokana na janga la virusi vya UVIKO 19 vilivyoikumba mataifa mbalimbali duniani.

"Huko nyuma ZIFF tulikuwa tunapokea filamu kati ya 400 hadi 500 na kuna wakati zilifikia hadi 1000. Tunaamini filamu hizi 65 zilikuwa bora zaidi na zimepata nafasi na tutarajie kuziona kwenye jukwaa letu la ZIFF2021, hiyo 21-25 Julai  mwaka huu katika majukwaa matatu tofauti ikiwemo; 

Jukwaa la Ngome Kongwe, Ukumbi wa Mpendae [Mpendae Mall], na ukumbi wa hoteli ya Maru maru pamoja na kwenye Jukwaa la Wanawake [Women Panorama] katika Vijiji mbalimbali.

Mwisho amewaomba wadau kuendelea kujitokeza kwa wingi kuweka udhamini ilikusaidia uwepo wake wa tamasha ambalo limezingatia katika kusaidia Wanawake kwenye tasnia ya filamu huku pia likilenga uchumi wa bluu kwa kuinua vipaji vya Vijana.



Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2