FORUMCC, UMOJA WA WASHIRIKIANA NA WANANCHI KUFANYA USAFI 'KAWE BEACH' | Tarimo Blog

Na Said Mwishehe,Michuzi TV

SHIRIKA la FORUMCC kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya(EU) kwa kushirikiana na Shirika la Forumcc ambalo limejikita katika kutunza mazingira pamoja na kukabiliana na mabadiliko ya TabiaNchi wamefanya usafi katika Fukwe ya Kawe(Kawe Beach) wilayani Kinondoni mkoani Dar es Salaam huku wakihamasisha jamii kushiriki kikamilifu katika kutunza mazingira yakiwemo ya fukwe ya Bahari ya Hindi.

Usafi wa fukwe hiyo umefanyika leo asubuhi ambapo wadau mbalimbali wa mazingira wameshiriki kwa kufanya usafi na kuzoa taka ngumu zilizopo maneo ya fukwe hiyo.

Akizungumza baada ya kufanyika kwa usafi huo, Katibu Tawala Wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam Sofia Msofe amesema FORUMCC na Umoja wa Ulaya wameonesha mfano nzuri kwa kufanya usafi eneo hilo la ufukwe wa Kawe hasa mtaa wa Mzimu, hivyo ni vema jamii ikawa na utamaduni wa kufanya usafi wa mazingira.

"Tunawashukuru FORUMCC na Umoja wa Ulaya kwa uamuzi huu wa kuja kufanya usafi na hii itatuamsha wananchi Kawe na Wilaya yetu ya Kinondoni kwa ujumla kuwa na utamaduni wa kufanya usafi,"amesema Msofe na kusisitiza kutunza mazingira ni wajibu wa kila mmoja wetu.

Kwa upande wake Balozi wa Irish nchini Tanzania Mary O'Niel amesema nchi yake na Umoja wa Ulaya wanatambua na kuthamini uhifadhi na utunzaji mazingira, hivyo wameona ni vema wakashirikiana na Shirika la FORUMCC na wadau wengine wa mazingira kufanya usafi kwenye fukwe hiyo.

"Tunalo jukumu la kulinda na kuhifadhi mazingira kutoka kizazi kimoja hadi kingine ili kuwakabidhi kikiwa safi lakini sio tu kukabidhi, bali tukabidhi hali ikiwa nzuri.Wakati tunafanya usafi hapa tulikuwa na watoto pamoja na jamii kwa ujumla, hivyo sote tunatakiwa kuhakikisha watoto hao wanakuja kukuta mazingira yakiwa kwenye uhalisia wake,"amesema.

Aidha amesema kuna haja pia ya kubadilisha tabia katika utunzaji mazingira na hilo ni jukumu la wote iwe mdogo au mkubwa"Nakumbuka zamani nikiwa na baba yangu tukisafiri kwa gari, tulikuwa tunafungua madirisha ya gari na kutupa uchafu nje lakini kwa sasa haiwezekani kwasababu mtazamo umebadilika".

Ameongeza kuwa nchi yake kupitia mpango kazi wake uliopo katika kutunza mazingira, itaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kufanikisha mipango iliyopo katika eneo hilo la mazingira.
Wakati huo huo Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania ambaye ni Mkuu wa Idara ya Ushirikiano C'edric Merel amessisitiza umuhimu wa kuhakikisha mazingira yanaachwa safi ikiwemo maeneo ya fukwe."Tutunze mazingira kwa kutotupa taka hovyo,Umoja wa Ulaya tunao mpango wa miaka saba na moja ya eneo ambalo tumelipa kipaumbele ni uhimili wa mabadilik ta tabianchi.

Amesisitiza katika mpango huo, utafanikiwa kwa jamii kufanya kazi kwa pamoja huku akieleza ni wajibu wa kila mmoja wetu kuwa sehemu ya kutunza mazingira.Pamoja na mikakati hiyo ameeleza wazi jamii isiwe sehemu ya kuchafua fukwe kwa kutupa taka hovyo.

Balozi wa Irish nchini Tanzania Mary O'Niel (aliyesimama) akizungumza baada ya FORUMCC na Umoja wa Ulaya kushirikiana kufanya usafi katika ufukwe wa Kawe mkoani Dar Salaam.
Wadau wa mazingira ambao wameshiriki kufanya usafi katika ufukwe wa Kawe uliopo kwenye Bahari ya Hindi wakiwa wameshika bendera ya Umoja wa Ulaya baada ya kumalizika kufanya usafi wa fukwe hiyo.FORUMCC na Umoja wa Ulaya(EU) ndio wameshirikiana kuandaa tukio hilo kwa kutambua umuhimuwa maeneo ya fukwe kuwa safi kimazingira.
Katibu Tawala Wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam Sofia Msofe aliyekuwa mgeni rasmi akizungumza mbele ya wadau wa mazingira wakiwemo wananchi wa Kawe ambao wameshriki kufanya usafi katika Ufukwe wa Kawe mkoani Dar es Salaam.
Sehemu ya wadau wa mazingira wakiwa makini kufuatilia maelezo yanayohusu umuhimu wa kutunza maeneo ya fukwe za bahari kutoka kwa viongozi waliohudhuria tukio la kufanya usafi katika Ufukwe wa Kawe.
Wadau wa mazingira wakimiminika takataka kwenye sandarusi baada ya kuziokota kwenye Ufukwe wa Kawe uliopo Bahari ya Hindi mkoani Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania ambaye ni Mkuu wa Idara ya Ushirikiano C'edric Merel akizungumza kuhusu umuhimu wa jamii kushirikiana katika kutunza mazingira ya fukwe za bahari.
Katibu Tawala Wilaya ya Kinondoni Sofia Msofe(kushoto) na Balozi wa Irish nchini Tanzania Mary O'Niel(wa pili kulia) wakipata maelezo ya aina ya takataka ambazo zinaonekana kuokotwa kwa wingi wakati wadau wakifanya usafi wa mazingira ya fukwe hiyo.
Wadau wa mazingira wakiweka ndoo ya kunawia maji katika Ufukwe wa Kawe uliopo Bahari ya Hindi kwa ajili ya kuwezesha wananchi wanaofanya shughuli zao katika fukwe hiyo kunawa mikono kama sehemu ya kukabiliana na janga la Covid -19 pamoja na kutunza mazingira.
Mhakiki na Mkaguzi wa takataka kutoka Taasisi ya Nipe Fagio Joseph Mkimbili(kulia) akitoa ufafanuzi wa aina ya taka ambazo zimeokotwa kwa wingi wakati wadau wakifanya usafi kwenye fukwe.
Katibu Tawala Wilaya ya Kinondoni Sofia Msofe(kushoto) na Balozi wa Irish nchini Tanzania Mary O'Niel(wa pili kulia) wakiangalia takataka ambazo zimeokotwa wakati wadau wa mazingira wakifanya usafi Kawe Beach.
Wadau wa mazingira wakichambua aina ya takataka ambazo zimeokotwa katika Ufukwe wa Kawe uliopo Bahari ya Hindi mkoani Dar es Salaam.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2