JAJI Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahimu Juma amewataka majaji wa mahakama ya Rufaa na Mahakama kuu kutoogopa kusema au kutoa taarifa katika vyombo husika wanapobaini mapungufu katika sheria.
Akifungua Mafunzo Elekezi kwa Majaji 31 wa Mahakama ya Rufaa na Mahakama Kuuu Tanzania Bara na Visiwani ambao waliteuliwa na kuapishwa hivi karibuni na Rais Samia Suluhu Hassan, Jaji Mkuu Juma pia aliwataka majaji kuzingatia maadili na uadilifu na kuweka Mungu mbele katika maamuzi yao kwa sababu maamuzi hayo yanagusa maisha ya watu wengi..
Akisisitiza juu ya jukumu kwa majaji kuwa watafsiri wakuu wa sheria alisema kuwa wanapokwenda kufanya kazi watakutana na mapungufu ya sheria.
“Kazi kubwa ya majaji ni kutafsiri sheria na Katiba. Tafsiri zetu za sheria na katiba.
Profesa Juma alisema kuwa Majaji wajielewe kuwa wao ni viongozi na sehemu ya maboresho hivyo wasikae kimya wanabaini mapungufu katika sheria ili zinfanyiwe maboresho kwa faida ya watanzania.
Alisema kuwa Katiba imewakopesha viongizi hao wa Mmahakama mambo Fulani na kubakisha mambo mengine ambayo ni haki za wananchi zinatokiwa kulindwa.
zielekezwe katika ustawi wa watu. katika Kila jalada utakalotolea hukumu unagusa maisha ya watu,”alisema Jaji Mkuu na kusisitiza umuhimu mkubwa wa majaji kufuata maadili na kuwa waadilifu.
Alisema watu wengi wanasema sheria zibadilishwe lakini ukweli ni kuwa sheria nyngi si mbaya bali wakati mwingine binafsi za watu ndio zenye matatizo.
Aliwataka majaji kuwa na tabia chanya na kwamba wananchi wana matarajio mengi juu yao kuhusu ulinzi wa haki zao..
Naye Jaji Kiongozi, Eliezer Feleshi alisea kuwa mafunzo hayo niya pili kufayika kwa Majaji Rufaa, ya sita kwa Majaji Mhakama Kuuu na mara ya Pili kwa majaji kutoka Tanzania Zanzibar.
Alisema kuwa mafuzo hayoyaaakisi sera ya mafunzo ya Mahakama na ni uthibitisho kuwa maboresho yanajengewa misingi bora ya utekelezaji.
Pia alisema kuwa mafunzo hayo ambayo yatakuwa na muenndelezo katika htua yapili ambapo majaji watapewa fursa ya kusikiliza na kuamua mashauri katika wiki mbili zijazo.
Alikisifu Chuo cha Mahakama kwa kuwa msaada kwa kuandaa mafunzo hayo yanayoongozwa na Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani, Jaji Salimu Masati.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment