Aliyasema hayo wakati akitoa mafunzo ya kuepukana na majanga katika shehia ili kujikinga na maafa huko katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kusini Makunduchi.
Amesema ni vyema kwa kila Sheha wa Shehia kujua maeneo hatarishi katika shehia yake ambayo mara nyingi hutokezea majanga na kuyaripoti sehemu husika kwa lengo la kupatiwa ufumbusu wa haraka ili kuepukana na maafa .
Alisema Masheha wana jukumu la kuhakikisha kuwa wananchi wanaishi katika maeneo salama yasiyokuwa na athari za viashiria vya majanga na kuyaepuka
“Jamii inapaswa kupewa elimu katika ngazi ya familia ili kuwajengea uwezo wa kufahamu athari zinazoweza kutokea pindipo wakiishi na viashirio vya majanga kama vile kuwepo miti mikubwa karibu na nyumba zao, mashimo yanayotuwama maji pamoja na wanaoishi sehemu ya njia za maji au mabondeni”, alieleza Mkurugenzi huyo. .
Hata hivyo alizitaka kamati za kukabiliana na maafa za shehia kutenga fedha zitakazosaidia katika hatua ya awali kwa mwananchi ambae atapatwa na janga la aina yeyote katika shehia yake .
Mkurugenzi huyo wa Divisheni aliwasisitiza wajumbe wa Kamati hiyo kufanya vikao vya mara kwa mara vitatoa maamuzi kwa makubaliano ya pamoja ya kuandaa mipango na taratibu sahihi za kukabiliana na maafa katika shehia zao .
Alifahamisha kuwa wajumbe wa kamati hiyo wana wajibu wa kuwasimamia utoaji wa huduma kwa wananchi ambao watatokezewa na dharura ya majanga au maafa ya mali kuwapatia msaada wa haraka na kuwanusuru .
Akitoa mafunzo ya Huduma ya Kwanza Katibu wa huduma hiyo Mkoa wa Mjini Magharibi Haji Ali Khamis aliwafahamisha masheha hao kwa njia ya vitendo jinsi ya majeruhi anavyosaidiwa katika hatua za awali kabla ya kufikishwa hospitali iwapo majeruhi wa ajali ya gari au wa kuzama baharini .
Nao Masheha hao waliomba kutayarishiwa kifungu maalum cha fedha ambazo zitasaidia yatakapotokea majanga makubwa katika shehia zao na kurahisisha kutatua matatizo kwa haraka.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment