MABINTI kutoka mikoa mitatu ya Dar es Salaam, Dodoma na Manyara wamepata fursa ya kunadi shughuli zaa maendeleo ya Serikali na jamii kupitia shindano la 'Miss Maendeleo' linalotarajiwa kufanyika mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Mkoani Dar es Salaam Mwenyekiti wa shindano hilo Moses Soud amesema, shindano hilo la kwanza kufanyika limelenga kuwainua mabinti ambao pia watakuwa mabalozi wa kutangaza shughuli za maendeleo zinazofanywa na Serikali na jamii kwa ujumla.
Amesema, shindano hilo litakalofanyika katika mikoa mitatu litahusisha mabinti wenye elimu kuanzia kidato cha nne, wenye akili timamu, watanzania wanaozungumza lugha mbili na zaidi na wenye umri kuanzia miaka 18-25 na baada ya washindi kutoka katika Mkoa kupatikana watachuana kumpata mshindi wa jumla na zawadi nono zitatolewa.
Amesema fomu za ushiriki zinapatikana katika chama cha waigizaji Ilala na Chuo cha Furahika Education College kilichopo Buguruni Malapa na tayari Wizara husika na baraza la sanaa la Taifa (BASATA,) wamebariki mashindano hayo.
Kwa upande wake mjumbe wa kamati ya mashindano hayo na mwigizaji wa filamu Diana William amesema hiyo ni fursa kwa mabinti ambayo itawasaidia kushiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii pamoja na kuibua vipaji vyao na amewashauri wazazi kuwaruhusu mabinti kushiriki katika mashindano hayo.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment