MTOTO WA IRENE UWOYA AMALIZA MAFUNZO YA KWANZA YA COMMUNION | Tarimo Blog

 


Na Leylah Nassib, DSJ

MTOTO wa msanii maarufu wa Filamu Irene Uwoya Krish Ndikumana amemaliza mafunzo yake ya kwanza ya communion siku ya jana jumapili na kufatiwa na sherehe kubwa ambayo ilifanyika  jioni hiyo na kuhudhuriwa na wasanii wakubwa akiwemo Diamond, Aunt Ezekiel ,Jackline Wolper Kajala na mwanaye paula na wengine wengi.

Mama mzazi wa krish, Irene uwoya aliwaeleza waandishi wa habari kuwa;  mafunzo ya communion ya krish aliyafanya kwa kipindi cha miezi sita na kumaliza siku ya jana lakini pia baada ya kuulizwa kwanini hakuonekana akifanya mafunzo hayo alieleza kwamba si kila kitu katika maisha yao ni lazima wakipost katika mitandao ya kijamii hasa mambo ya Mungu na alimaliza kusema anafuraha kubwa na kumshukuru sana Mungu mtoto wake kupata mafunzo hayo.

Licha ya sherehe hiyo pia kulikua pia na maneno mengi pamoja na maoni mengi  kumhusu mtoto huyo kuhusu (mtindo)style yake ya unyoaji kwamba Mama yake hakustahili  kumnyoa style hiyo kwani ni kinyume na maadili yao ya kikanisa na kupitia comments hizo Irene uwoya aliweza kujibu kua Mungu anaangalia moyo na sio kuzungumia style hiyo ya unyoaji kwani ukristo haupo kwenye nywele wala kwenye mavazi ya mtoto wake hivyo hajali watu wakisema.


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2