MBUNGE wa Mtama Nape Nnaye amesema kuwa Serikali ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Mhe Samia Suluhu Hassan ni mfano wa Serikali sikivu hasa kwa kutoa nafasi ya kutoa muda wa kufafanua masuala mbalimbali ya Wananchi.
Akizungumza katika kikao cha wadau wa korosho kilichowakutanisha na Waziri Mkuu, Nape amesema, Wananchi wa Lindi wamepokea kwa mikono miwili na furaha uamuzi wa Rais Samia wa kuamua kuwatua wakulima wa korosho shilingi 110 baada ya maombi yao waliyowasilisha kama wawakilishi wa wananchi.
Nape amesema kuwa, Mamlaka ya mapato (TRA,) mkoani Lindi walitoa taarifa ya kuanza kukatwa kodi kwa wakulima wa mazao ya biashara wenye mapato yanayoanzia shilingi milioni nne na kuwataka wakulima hao kupeleka makisio ili waanze kukatwa kodi jambo lililozua taharuki kwa wakulima hasa wakorosho.
Amesema, licha ya kuwepo kwa makato mengi kwa zao la korosho, TRA wakaja na sheria ya kukata kodi zaidi kwa wakulima hao kwa sheria ambayo ni kandamizi ambayo Serikali haina budi kufuta na kuiondoa kabisa.
Kuhusu pembejeo za kilimo Nape amesema bado hazitoshelezi licha ya Sensa ya kilimo kufanyika kwa wakulima hao.
Vilevile ameiomba Serikali kuharakisha malipo ya fedha kwa wakulima na ameishukuru Serikali kwa kuendelea kutoa muda wa kwenda kukutana na wakulima na kufafanua kuhusu jambo hilo.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment