SERIKALI KUITUA MZIGO ATCL | Tarimo Blog

Na Farida Saidy, Morogoro
SERIKALI imeahidi kulipa madeni yote wanayodiwa na shirika la ndege Tanzania ATCL ili kuhakikisha shirika hilo linajikwamua kiuchumu na tayari mikakati ya ufnikisha hilo imeshapangwa ,huku ikiwatoa hofu watanzania kuwa shirika lipo imara na litaendelea kutoa huduma kwa wananchi.

Akizungumza na wafanyakazi wa shirika hilo mjini Morogoro,Naibu Waziri Wizara ya ujenzi na uchukuzi, Godfrey Kasekenya amesema maamuzi hayo ya Serikali yatalifanya shirika hilo kujiendesha kwa faida na kuleta tija kwa wafanyabishara wa ndani na njee ya nchi wanaotegemea usafiri wa unga.

Aidha amesema Serikali itaendelea kuweka fedha katika shirika hilo ili kuboresha ufanisi na utendaji kazi utakaosaidia kukuza usafiri wa anga nchini na kuwavutia wasafiri kutokana na huduma mbalimbali zinazoendelea kutolewa.

Katika hatua nyingine amesema serikali kupia ATCL haitamfumbia macho wakala yeyote atakaye ficha mawasiliano ya mteja atakaye muhudumia,kwani kufanya hivyo ni kumnyima haki mteja ya kupata taarifa muhimu kutoka kwenye shirika jambo ambalo hutaleta usumbufu kwa wateja pale panapotokea kusitishwa au kubadilishwa muda wa safari.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa shirika la ndege Tanzania ATCL ameeleza mikakati ya kuboresha huduma za usafiri katika maeneo mablimbali ya ndani na nje ya nchi.

Aidha ameongeza kuwa pamoja na changamoto ya ugonjwa wa korona shirika litaendelea kujiimarisha kwa kutoa huduma zilizo bora na kuzingatia viwango vilivyowekwa kimataifa.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2