Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
MABINGWA Watetezi wa Michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports Federation Cup (ASFC), Simba SC wametua mjini Songea mkoani Ruvuma tayari kwa mchezo wao wa Nusu Fainali ya Michuano hiyo dhidi ya Azam FC mchezo utakaopigwa kwenye dimba la Majimaji June 26, 2021.
Simba SC watamenyana na Azam FC katika mchezo huo wakati Young Africans wenyewe wakicheza na Biashara United ya Mara mchezo utakaopigwa kwenye dimba la Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora, June 25, 2021 siku ya Ijumaa.
Kuelekea michezo hiyo, Simba SC na Young Africans wamevunja rekodi katika mapokezi yao baada ya kutua kwenye Mikoa hiyo, Simba SC (Songea) na Yanga SC (Tabora) wakati Azam FC wao wakielekea kimya kimya Songea kuwakabili Simba SC.
Wanajeshi wa Mpakani, Biashara United haijafahamika kama wametua Tabora au la! bali wamewataka mashabiki wao kujitokea kwa wingi katika dimba hilo la Ali Hassan Mwinyi ili kuwaangamiza Wananchi katika mchezo huo.
Simba SC wamefuzu hatua ya Nusu Fainali ya Michuano hiyo baada ya ushindi wa bao 3-1 dhidi ya Dodoma Jiji FC mchezo uliopigwa kwenye dimba la Benjamin Mkapa, wakati Young Africans wenyewe wakipata ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Mwadui FC mchezo uliochezwa kwenye dimba la CCM Kambarage, Shinyanga.
Biashara United walifika hatua hiyo walipopata ushindi wa bao 2-0 dhidi Namungo FC mchezo uliopigwa kwenye dimba la Kumbukumbu ya Karumbe mkoani Mara, Azam FC walifuzu Nusu Fainali kwa ushindi wa bao 3-1 dhidi ya Rhino Rangers ya Tabora katika mchezo uliopigwa kwenye dimba la CCM Kambarage, Shinyanga.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment