TPA YAZINDUA KITUO MAALUM KWA AJILI YA KUHUDUMIA WATEJA KWA NJIA YA SIMU | Tarimo Blog


Na Said Mwishehe, Michuzi TV.


MAMLAKA ya Bandari Tanzania(TPA) imeamua kusogeza huduma zake karibu zaidi na wananchi ambao sasa imezindua rasmi kituo maalum kwa ajili ya kuhudumia wateja kwa njia ya simu ya mkononi ambapo kituo hicho kitatoa huduma kwa saa 24.

Akizungumza katika uzinduzi wa kituo hicho cha TPA Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Leonard Chamuriho amesema hatua hiyo ni ishara ya kuendeleza kazi katika Serikali ya Awamu ya Sita chini ya kiongozi mahiri Rais Samia Suluhu Hassan katika kuendelea kuwahudumia wananchi.

Amesema ili wananchi wanaohitaji kupata huduma za TPA watatakiwa kupiga namba ya simu 0800110032 muda wowote na kisha watahudumiwa na kwamba hakuna gharama yoyote kwa watakaokuwa wakiitumia , kwani lengo ni kusogeza huduma iwe ndani au nje ya nchi.

Aidha Mhandisi Chamuriho amewapongeza TPA kwa hatua hiyo ya kujali wateja wa ndani na nje kwa kuhakikisha wanapata huduma stahiki kupitia Mamlaka hiyo."Hatua hii ya TPA ni ya kupongeza kwani tumeelezwa hapa huduma zitatolewa saa 24, mtu anapopata tatizo lolote na wakati wowote anayo nafasi ya kuwasiliana na TPA moja kwa moja."

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TPA Eric Hamissi ameahidi kutoa huduma kwa saa 24 kupitia Kituo hicho huku akieleza kwamba kituo hicho kinakuja kondoa changamoto ya wale ambao waliihitaji kupata huduma za TPA lakini hakuwa na njia ya haraka ya kuwasiliana nao, hivyo sasa kwa kutumia namba hiyo ya simu itakuwa rahisi kwa yoyote kuwasiliana nao.

"Namba ambayo itatumika kwa kwenye kituo hiki ni 0800110032, haina gharama kwani gharama zote zimeshalipiwa na TPA, hivyo huduma hii ni bure na tunaamini inakwenda kutatua changamoto papo kwa hapo kwa wale ambao watakuwa na changamoto yoyote na inahitaji ufumbuzi wetu,"amesema Hamissi.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Dk.Leonard Chamuriho (katikati) na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA) Profesa Ignatus Rubaratuka(kushoto) wakikata utepe kuashiria kuzinduliwa kwa kituo maalum cha TPA kwa ajili ya huduma kwa wateja.Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TPA Eric Hamissi.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Dk.Leonard Chamuriho(katikati aliyeshika kipaza sauti) akiuliza swali kwa mmoja ya watoa huduma kwa wateja katika kituo hicho maalum kwa ajili ya kuhudumia wateja baada ya kukizindua rasmi leo Juni 25,2021.Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa TPA Eric Hamissi na kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA) Profesa Ignatus Rubaratuka.Waliokaa ni watoa huduma kwa wateja wa kituo hicho.
Mmoja ya watoa huduma kwa wateja katika kituo hicho maalum ya TPA akitoa maelezo ya jinsi wanavyoweza kupokea simu za wateja na kuwahudumia kwa Waziri Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Dk.Leonard Chamuriho(katikati).
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania Eric Hamissi(wa kwanza kushoto)Waziri Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Dk.Leonard Chamuriho(katikati) na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA) Profesa Ignatus Rubaratuka(kulia) wakishangilia baada ya kuzinduliwa kwa kituo maalum kwa ajili ya kuhudumia wateja wa TPA kwa njia ya simu.
Waziri Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Dk.Leonard Chamuriho akizungumza wakati akizindua kituo maalum kwa ajili ya huduma kwa wateja wa TPA ambao watahudumia kwa njia ya simu kokote waliko kwa kupiga namba ya simu ambayo haina gharama yoyote lengo ikiwa kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi.
Watoa huduma kwa wateja katika kituo hicho maalum wakiendelea na utoaji huduma kwa njia ya mawasiliano ya simu baada ya kuzinduliwa kwa kituo hicho.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Eric Hamissi akifafanua kuhusu kituo hicho maalumu cha kuhudumia wateja kwa njia ya mawasiliano ya simu wakati wa uzinduzi wa kituo hicho.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Dk.Leonard Chamuriho (katikati) akiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA) Profesa Ignatus Rubaratuka(kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa TPA Eric Hamissi(kushoto) wakijadiliana jambo wakati wa uzinduzi wa kituo hicho.
Sehemu ya wakuu wa idara mbalimbali za Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi pamoja na Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA) wakifuatilia kwa makini maelezo kuhusu kituo hicho ambavyo kitakuwa kikitoa huduma kwa wateja wakati kikizinduliwa rasmi.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Dk.Leonard Chamuriho akisaini kitabu cha wageni baada ya kufika Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA) kwa ajili ya kuzindua kituo maalum cha kuhudumia wateja kwa njia ya mawasiliano ya simu.(PICHA  NA SAID MWISHEHE)
 

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2