UNYWAJI WA POMBE KWA WANANCHI IRINGA KUNACHAGIA KUONGEZEKA KWA UDUMAVU KWA WATOTO | Tarimo Blog

Meneja wa shirika lisilo la kiserikali la Save the Chidren mkoani Iringa John Masenza akiongea na washiriki wa mkutano wa wadau wa kutafuta njia za kupunguza udumavu mkoani Iringa.
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa wadau wa kutafuta njia za kupunguza udumavu mkoani Iringa.
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa wadau wa kutafuta njia za kupunguza udumavu mkoani Iringa.

Na Fredy Mgunda, Iringa.
UNYWAJI wa pombe na kutokuwa na elimu ya lishe kwa baadhi ya wananchi wa mkoa wa Iringa kumetajwa kusababisha udumavu kwa watoto wadogo kutokana na wazazi wengi kutozingatia kuwapatia vyakula vyenye lishe bora.

Akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa kutafuta njia ya kutatua tatizo la kuongezeka kwa udumavu,meneja wa shirika lisilo la kiserikali la Save the Chidren mkoani Iringa John Masenza alisema kuwa wananchi wa mkoa wa Iringa wanakunywa sana pombe na kusahau swala la chakula kwa familia yake.

Alisema kuwa mkoa wa Iringa ni mmoja ya mkoa ambao unazalisha chakula kwa wingi lakini tatizo kubwa limekuwa kwa wananchi kuuza mazao hayo na kwenda kunywa pombe huku akisahau jukumu lake la kuwapatia watoto chakula chenye lishe bora.

Masenza alisema kuwa wananchi wanapokunywa pombe kwa wingi mara nyingi husahau kabisa swala la kwenda kula kutokana na kuwa tayari anakuwa amelewa na hata kusahau kuwapikia chakula watoto wadogo ambao aliwaacha nyumbani.

“Kumekuwa na tabia moja ya wazazi kwenye vilabuni au kwenye bara na watoto wadogo na kuwanywesha pombe jambo ambalo linapelekea watoto kupoteza hamu ya kula na kusababisha udumavu kwa mtoto” alisema Masenza

Masenza alisema kuwa mradi wa USAID lishe endelevu umejipanga kuhakikisha unachangia kupunguza udumavu kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano kwa lengo la kuboresha mifumo mbalimbali ya lishe.

Alisema kuwa lengo la mradi wa USAID lishe endelevu umejipanga kuhakikisha kuwa wanapunguza udumavu kwa asilimia kumi na tano kwa kutoa elimu na kuboresha mifumo mbalimbali iliyopo katika maeneo ambayo mradi unafanyika.

Kwa upande wake kaimu katibu tawala wa mkoa wa Iringa,Elia Luvanda alisema kuwa mkoa wa Iringa unashika nafasi ya tatu kitaifa kwa mikoa ambayo inaudumavu wa watoto wadogo kutokana na wananchi wengi kutokuwa na elimu ya lishe.

Luvanda alisema kuwa hali ya udumavu kwa watoto wadogo mkoani Iringa ipo kwenye asilimia 47 hali hii sio nzuri kabisa kwa maendeleo ya kuwa na kizazi cha bora hapo baadae hivyo wamejipanga kuhakikisha wanaboresha mifumo ya kiserikali ili kutoa elimu ya lishe bora kwa wananchi wote.

Naye afisa lishe wa wilaya ya Kilolo mkoani Iringa Fanuel Nyandwike alisema kuwa wilaya hiyo inashida kubwa ya watoto wengi kuwa na utapiamulo na kupelekea kuongezeka kwa udumavu kwa watoto waliopo katika wilaya hiyo.

Alisema kuwa sababu kubwa ya kuongezeka kwa udumavu inatokana na wazazi wengi kuwa walevi wa kupindukia na kusahau majukumu ya kumulea mtoto kwa kumpatia chakula bora ambayo kina lishe ambacho kitachochea kupuza udumavu kwa watoto.

Nyandwike alisema kuwa uongozi wa halmashuri ya wilaya ya kilolo umejipanga kuhakikisha kila kijiji kinakuwa na sheria ndogo ya kuzibiti udumavu kwa kuwalazimisha wazazi kuzingatia kuwapatia watoto chakula chenye lishe bora.


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2