PAPAA MSOFE AACHIWA HURU | Tarimo Blog

Na Karama Kenyunko Michuzi TV
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru mfanyabiashara Marijan Msofe maarufu kama Papaa Msofe na wenzake wanne waliokuwa wakishtakiwa na mashtaka matano likiwemo la kujipatia Sh. Milioni 943 kwa njia ya udanganyifu baada ya Mkurugenzi wa mashtaka nchini (DPP) kudai kuwa hana nia ya kuendelea na mashtaka dhidi yao.

Mbali na Msofe, washtakiwa wengine ni Wenceslau Mtui, wakili wa kujitegemea Mwesigwa Mhina, Josephine Haule na Fadhil Mganga.

Msofe na wenzake hao ambao wamekaa mahabusu tangia 2019 wameachiwa kufuatia DPP, kuwasilisha hati (Nolle Prosque) kuonesha kuwa hana nia ya kuendelea na mashtaka dhidi yao chini ya kifungu cha sheria cha 91(1) ya makosa ya jinai (CPA).

Mapema, leo Juni 18, 2021 Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kuwa kes leo ilitwa kwa kutajwa na pia DPP ametoa hati ya nia ya kutokuendelea na mashtaka dhidi ya washtakiwa hao.

Katika kesi hiyo, washtakiwa hao walikuwa wakituhumiwa kuongoza genge la uhalifu na kufanya mpango wa kutekeleza kosa la kijinai.

Pia walidaiwa kutakatisha Dola za Marekani 300,000, sawa na Sh. Milioni 690 kutoka kwa Pasco Camile, wakati akijua ni zao la udanganyifu.

Pia walidaiwa kwa njia ya udanganyifu kujipatia kiasi Sh. Milioni 253 kutoka kwa John Mahsson kwa kumdanganya kuwa watamuuzia dhahabu kilogram 220 na kuzisafirisha kwenda nchini Ureno.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2