WAFANYABIASHARA KIZIMBANI KWA KIJIFANYA TISS MBELE YA DPP | Tarimo Blog

WAFANYABIASHARA Joshua Jelemia (37) na Yahaya Abdallah (31) wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na shtaka moja la kujifanya Usalama wa Taifa (TISS) kwa Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) na Naibu DPP.

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa Serikali Mwandakizi, Wankyo Simon mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Godfrey Isaya, imedai Juni 12,2021 katika ofisi za DPP zilizopo katika jengo la Wizara ya Mambo ya Ndani ndani ya Wilaya ya Ilala jijini Dar

Imedaiwa, siku na mahali hapo, washitakiwa hao walijitambulisha kwa DPP Slyvester Mwakitalu na Naibu DPP Joseph Pande kwamba wao ni maofisa kutoka TISS huku wakijua kuwa siyo kweli.

Hata hivyo, washtakiwa wamekana kutenda kosa hilo na wamerudishwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ambapo mahakama imemtaka kila mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili wa kuaminika kwa watakaosaini bondi ya sh. Milioni saba

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo umeishakamilika. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 22, 2021 kwa ajili ya washtakiwa kuja kusomewa maelezo ya awali.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2