UPEKUZI WA WATEULE NI ENDELEVU - DKT. NCHEMBA | Tarimo Blog



Na, Saidina Msangi, WFM, Dodoma

SERIKALI  imesema kuwa siyo sahihi kuwa na Kanzidata ya Upekuzi (Benki ya Waliopekuliwa) ili kurahisisha mchakato wa upekuzi kwa kuwa utendaji na mienendo ya maafisa hubadilika kuendana na wakati husika.


Hayo yameelezwa bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), alipokuwa akijibu swali la Mheshimiwa Jerry William Silaa, Mbunge wa Ukonga alieitaka Serikali kuanzisha Benki ya waliopekuliwa kwa ajili ya uteuzi ili kurahisisha zoezi la uteuzi wa Bodi za Taasisi na kuziwezesha Taasisi hizo kwenda na kasi ya Mhe. Rais kwa kile alichosema kuwa upekuzi umekuwa kisingizio cha kuchelewesha uteuzi.


“Upekuzi kwa ajili ya kujaza nafasi mbalimbali hufanyika kwa wakati husika kutokana na ukweli kwamba utendaji na mienendo ya maafisa pia hubadilika kutoka wakati mmoja hadi mwingine,” alifafanua Mhe. Nchemba.


Aidha, alieleza kuwa Wizara ya Fedha na Mipango ina jumla ya Taasisi 28 ambazo inazisimamiakati ya hizo, Taasisi Tisa (9) Bodi zake zimemaliza muda wake.


Mhe. Nchemba alisema kuwa mapendekezo ya majina kwa ajili ya kujaza nafasi za Wenyeviti na Wajumbe wa Bodi hizo yamewasilishwa kwenye Mamlaka za Upekuzi.


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2