MRATIBU wa mafunzo hayo kutoka taasisi ya teknolojia ya Dar es salaam, (DIT), Bahari Hababuu akizungumza na wachimbaji wa madini ya Tanzanite Mji mdogo wa Mireani, amesema mafunzo hayo yatafanyika Juni 7 jijini Dar es salaam, kwa muda wa wiki mbili.
Hababuu amesema mafunzo hayo yatawasaidia wadau wa madini kufanya kazi zao za uchimbaji na ulipuaji kwa ubora, uhakika na usalama zaidi tofauti na awali.
Amesema mafunzo hayo yatahusisha mambo mbalimbali ikiwemo masuala ya usalama, utumiaji wa vifaa vya kisasa na utumiaji wa njia za uchimbaji wa kisasa kutoka kwa wataalamu wa chuo cha DIT.
“Ni fursa nzuri kwa wadau wa madini kushiriki mafunzo hayo ya wiki mbili yatakayoanza Juni 7 hadi Juni 18 kuanzia saa tisa alasiri hadi saa moja jioni,” amesema Hababuu.
Wakili wa kampuni ya kisheria ya L & L Attorney @ law, Faisal Rukaka, akizungumza na wachimbaji hao wa madini ya Tanzanite, amesema suala la wadau wa madini ya Tanzanite kuwa na wanasheria halikwepeki.
Rukaka amesema wachimbaji wanapaswa kushirikiana na serikali na wao wanasheria ili kujengewa uwezo wa masuala mbalimbali ikiwemo namna ya kupata vibali mbalimbali.
Amesema serikali ni mlezi wao wadau wa madini ila wanapaswa kuwa na wanasheria watakaoweza kuwapa elimu ikiwemo ya uchimbaji, kodi, leseni na mambo mbalimbali.
Amesema kutokujua sheria siyo utetezi wa kufanya kosa hivyo kupitia wanasheria wanaweza kushirikiana na wahusika wa fani husika ikiwemo wanasheria ili kuendeleza kazi zao kwa mapana zaidi.
“Kunakuwepo na makosa madogo madogo ambayo wangekuwa na wanasheria wangeweza kunufaika juu ya masuala ya kisheria na shughuli zao kwenda vizuri inavyopaswa,” amesema Rukaka.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment