WANANCHI IRINGA WAFURAHIA HAPPINESS SENADA KUBAKIA KUWA KATIBU TAWALA IRINGA. | Tarimo Blog



Katibu tawala wa mkoa wa Iringa Happiness Seneda akiwa kwenye majukumu yake ya kikazi mkoani Iringa (PICHA KUTOKA mAKTABA)

Na Fredy Mgunda,Iringa.



Wananchi wa mkoa wa Iringa wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suruhu Hassan kwa kumbakisha katibu tawala Happiness Senada kuendelea kuwa kiongozi wa mkoa huo kutoka utumishi bora alioufanya toka ateuliwe katika awamu ya tano.

Wakizungumza na blog hii wananchi wa wilaya ya Iringa walisema kuwa katibu tawala Seneda amefanikiwa kutekeleza vilivyo ilani ya chama cha mapinduzi yam waka 2015/2020 kwa kuteleza shughuli za kimaendeleo vilivyo akishirikiana na aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hpai.

Walisema kuwa Seneda amefanikiwa kutatua migogoro mingi ambayo imemfikia mezani kwake hata ile iliyokuwa ilishindikana kwa viongozi wengine lakini yeye anakuwa anaishughulia kwa sheria,busara na hatima kupata ufumbuzi wa migogoro mbalimbali.

“Huyu ni kiongozi mwenye busara sana na anajua kuwa kitu gani anafanya ili kuhakikisha anakuza uchumi wa mkoa wa Iringa na kuleta maendeleo kwa kusimamia miradi mbalimbali ya kimkakati iliyopo mkoani hapa” walisema wananchi

Wananchi hayo waliongeza kuwa amekuwa msaada mkubwa wa kumsaidia mkuu wa mkoa kwenye shughuli mbalimbali kama kukuza uchumi,kuboresha sekta ya afya,miundombinu,kilimo,elimu,mazingira,ardhi na ndio sababu ya mkoa wa Iringa kufanya vizuri karibia kila sekta.

Walisema kuwa amekuwa hasikiki mara kwa mara kwenye vyombo vya habari lakini amekuwa kiongozi mwenye maono ya mbali ya kukuza uchumi na kuleta maendeleo ya mkoa wa Iringa akishirikiana vizuri na viongozi wa ngazi za chini bila kumbagua kiongozi au mfanyakazi yeyote yule.

Kwa upande wa wananchi wa wilaya ya Mufindi walisema kuwa uchumi wa wilaya hiyo unaimarika kila uchwao kutokana na uongozi bora wa katibu tawala kwa kuwapatia fursa wawekezaji na wafanyabiasha kufanya shughuli zao bila kuwa na kusumbuliwa bali kwa kufuata sheria na katiba ya nchi.

Walisema kuwa toka amefika mkoa wa Iringa amefanikiwa kutoa fursa kwa wawekezaji wengi kwenye sekta mbalimbali katika wilaya hiyo na ndio sababu ya kuonmgezeka kwa viwanda vingi na kukua kwa uchumi wa wananchi wa wilaya hiyo.

“Tunamuomba aongeze kasi ya kubuni mbinu mbalimbali za kukuza uchumi,utawala bora na kuleta maendeleo kwa wananchi wa mkoa wa Iringa baada ya Mheshimiwa Rais kumbakiza kuwa kiongozi kwenye mkoa wa Iringa” walisema wananchi wa Mufindi

Aidha walimta katibu tawala Happiness Seneda kuhakikisha anaendelea kutoa ushirikiano kwa mkuu wa mkoa mpya kama alivyofanya kwa mkuu wa mkoa aliyepita ili kutatua changamoto na kukuza uchumi na kusimamia utawala bora kwa watumishi wa UMMA.

Nao wananchi wa wilaya yay a Kilolo walimpongeza katibu tawala kwa kuwa kiongozi shupavu kwa kutatua kero za wananchi mara baada ya kutenga siku ya alhamisi kuwa siku ya kuwasikiliza wananchi ofisini kwake.

Walisema kuwa kila mwananchi wenye kero akikutana na katibu tawala huyo atapa namna ya kutatuliwa kero zao kwa kuwasikiliza kila mmoja kwa nafasi yake na kufanikiwa kuzitatua kero kwa kiasi furani japo bado kunachangamoto nyingi hazijatatuliwa kwa wananchi wa mkoa wa Iringa.

Wananchi hao wa wilaya ya kilolo walimuomba katibu tawala kwa kushirikiana na mkuu wa mkoa wa Iringa Queen Sendiga kuhakikisha wanatatua chngamoto za miundombinu ambayo imekuwa ikirudisha nyuma maendeleo ya wananchi wa wilaya hiyo.

“Huku Kilolo kuna fursa nyingi sana za kiuchumi ila tatizo la miundombinu ya barabara linatukosesha kukuza uchumi,kupata maendeleo kwa haraka na kukosa wawekezaji wengi kutokana natatizo hilo hivyo tunaombawatusaidie kutafuta njia ya kutatua tatizo hilo lisijirudie tena” walisema wananchi wa Kilolo

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2