WAZIRI wa Maji Mhe.Jumaa Aweso,akizungumza wakati akifungua kikao kazi cha watendaji wa wizara ya maji na taasisi zake katika kada ya manunuzi na ugavi, uhasibu na wakaguzi wa ndani kilichofanyika leo Julai 8,2021 jijini
Aweso amesisitiza watumishi hao kuachana kabisa na michakato isio na ulazima inayochelewesha miradi ya Maji na kuwataka kujipanga vilivyo katika kufanikisha utekelezaji wa miradi kwa haraka na viwango.
Aweso amewataka watumishi hao kwenda kufanya kazi kwa mujibu wa sheria,kanuni na taratibu zilizowekwa huku akiwasisitiza zaidi kutenda haki,kuzingatia nidhamu na kuboresha mahusiano mazuri katika utekelezaji wa majukumu yao.
‘’Pasipo na nidhamu mipango mizuri haiwezi kufanikiwa nidhamu ianze kwa mtu mmoja mmoja, dhamira yetu kwenye wizara ya maji ni kuhakikisha miradi ya maji itekelezwe kwa ubora na kumalizika kwa wakati”amesema Aweso
Aidha, Aweso amesema kuwa ukiacha Bajeti ya sh Bilion 680 waliopewa na Serikali,Rais Samia amewaongezea sh billion 207 ili kuboresha sekta ya Maji kwa sababu ameipa kipaumbele.
‘’Tusishangilie tu kuwa tumeongezewa fedha halafu mkajenge mianya ya kutumia fedha vibaya,hizi fedha haziliki ,ukiamua kula kwa makusudi hizi fedha za mama Samia jela inakuita’’amesisitiza Aweso
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment