BoT YATOA ELIMU YA HUDUMA ZA KIFEDHA KWA WANANCHI KWENYE MAONESHO YA SABASABA JIJINI DAR ES SALAAM | Tarimo Blog

Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania, Bw. Edwin N. Rutageruka (kushoto), akipewa elimu na Mchambuzi wa Masuala ya Fedha, Bw. Martin Kalihose,  kuhusu namna ya kuwekeza katika Dhamana za Serikali za muda mfupi (Treasury Bills) na muda mrefu (Treasury Bonds) alipotembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwenye Maonesho ya Sabasaba jijini Dar es Salaam. 

Mkaguzi wa Benki Mwandamizi, Bw. Gideon Rwegoshora (kulia), akifafanua jambo kuhusu Usimamizi wa Sekta ya Fedha kwa wananchi alietembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwenye Maonesho ya Sabasaba jijini Dar es Salaam. 

Mhasibu Mkuu Mwandamizi, Bw. Elirehema Msemembo (katikati) akielezea kuhusu Huduma za Kibenki kwa mwananchi alietembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwenye Maonesho ya Sabasaba jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Meneja Msaidizi Idara ya Sarafu, Bw. Nixon Kyando na Afisa Benki Mkuu Mwandamizi, Bi. Restituta Minja. 

Afisa Uhusiano wa Umma, Bi. Beatrice Ollotu akiwaelezea wananchi huduma zinazopatikana katika banda la Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwenye Maonesho ya Sabasaba, yanayoendelea jijini Dar es Salaam. 

Afisa Rasimali Watu Mwandamizi, Bi. Joyce Shala, akifafanua jambo kuhusu Bodi ya Bima ya Amana (DIB). Kushoto kwake ni Afisa Benki, Bi. Rukia Muhaji. 

Mchambuzi wa Taasisi Mwandamizi, Bw. Peter George, akielezea masuala ya Utumishi na Uendeshaji ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwa wananchi. Kulia kwake ni Afisa Rasimali Watu Mwandamizi, Bi. Consolata Shao na Meneja Msaidizi Masomo ya Muda Mrefu kutoka Chuo cha BoT Mwanza, Bw. Airenus Mlowe

Meneja Msaidizi Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki, Bi. Victoria Msina, akizungumza na wananchi waliotembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwenye Maonesho ya Sabasaba jijini Dar es Salaam. 

Mchambuzi wa Mifumo, Bw. Robert Masalu na Mchambuzi wa Fedha Mwandamizi, Bi. Kidee Mshihiri katika mazungumzo na mwananchi kuhusu Mifumo ya Malipo. 

Meneja Msaidizi Masomo ya Muda Mfupi kutoka Chuo cha BoT Mwanza, Bi. Tulla Mwigune, akigawa vipeperushi kwa wanafunzi waliotembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwenye Maonesho ya Sabasaba jijini Dar es Salaam. 

Afisa Uhusiano Mkuu Mwandamizi, Bi. Noves Moses, akizungumza na wananchi waliotembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwenye Maonesho ya Sabasaba jijini Dar es Salaam. 

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2