Na Farida Said, Morogoro.
Katika kuhakikisha wakulima wanakuwa na uhakika wa matibabu pindi wanapopatwa na maradhi, banki ya CRDB kwa kushirikiana na Mfuko wa Taifa Bima ya Afya (NHIF) wameanzisha utaratibu wa kuwawezesha wanachama wa AMCOS na familia zao kupata matibabu hospitalini kwa kutumia Bima ya afya kwa gharama nafuu mkoani hapa.
Akizungmza wakati wa utiaji saini makubaliano baina ya Banki ya CRDB, Mfuko wa Taifa Bima ya Afya (NHIF) na viongozi wa AMCOS za wakulima wa Miwa wa Wilaya ya Kilombero, Kaimu Meneja mkuu wa Banki ya CRDB, Wilson Mnzava Amesema CRDB inatambua changamoto za wakulima hususani katika Afya ndio maana imekuja na mkopo wa Bima ya Afya kwa wanaushirika, ambapo mkopo huo utatolewa bila ya Riba.
Mnzava amesema kuwa wanufaika wa Ushirika Afya ni wanachama wa AMCOS zote Tanzania pamoja na Familia zao ambapo watalipa shilingi 76,800 kwa mtu mzima na 50,400 kwa mtoto itakayowawezesha kupata matibabu Tanzania nzima ndani ya miezi 12 (mwaka mmoja).
“CRDB tunajua umuhimu wa miwa na sukari hapa nchini ndio maana tumewaleta ushirika afya ili muwe na uhakika wa afya zenu pamoja na matibabu ili muendelea kulima na kuongeza uzalishaji wa miwa”. Alisema Mnzava.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi huduma za wanachma kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Hipoliti Lello alisema kuwa upatikana wa Bima hiyo utawasaidia kuondoa usumbufu na michango ya matibabu isiyokuwa rasmi iliyokuwa ikijitokeza kwenye vyama vya ushirika hasa inapotokea mmoja wa wanachama akipatwa na maradhi.
“Ushirika Afya itawapunguzia michango midogo midogo mliokuwa mnachangishana kwenye vyama vyenu ikitokea mwezenu anaumwa au anauguliwa”. Alisema Lello.
Aliongeza kuwa kuna yale maswala ya njoo univunie mimi kwanza mtoto wangu anaumwa yataisha kama wanachama watajiunga kwenye Ushirika Afya, huku akiwahakikishia kuwa NHIF itakuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wanapata huduma bora.
Hata hivyo Kaimu Meneja wa Banki ya CRDB, Wilson Mnzava amesema kuwa Banki hiyo itaendelea kushrikina na wakulima, ambapo kwa mwaka wa Fedha wa 2021 Banki imetoa mikopo kwenye sekta ya kilimo ya shilingi Bilioni 735 sawa na asilimia 43 ya mikopo yote iliyotolewa na CRDB nchini.
Ameongeza kuwa Kati ya mikopo hiyo shilingi Bilioni 494 zimeelekezwa kwenye mazao makuu ya kimkakati na kusaidia zaidi ya AMCOS 472 kupata mikopo kwa ajili ya kuongeza tija katika uzalishaji kwenye kilimo.
Aidha mikopo hiyo imetolewa kwenye ununuzi wa pembejeo, Ujenzi wa Maghala na viwanda vya kuchakata mazao vitaavyo saidia kuongeza mnyororo wa thamani kwenye mazao yanayozalishwa hapa nchini.
Sambamba na hayo ametoa wito kwa wakulima wadogo kujiunga na Banki ya CRDB ili waweze kujikwamua kiuchumi na kupata mazingira wezeshi katika uzalishaji wa mzao.
Keneth Shemdoe ni mrajisi msaidizi wa vyama vya ushirika Mkoa wa Morogoro amevitaka vyama hivyo kuacha tabia ya kuvuruga utaratibu wa uvunaji wa miwa kwa sababu ya kukosa fedha za matibabu badala yake watumie bima za Afya kwenye matibabu.
Nae Makamu Mwenyekiti wa Miwa AMCOS Masoud Mkinga akizungumza kwa niaba ya viongozi wa wakulima wa miwa amesema wao kama viongozi wapo tayari kutoa elimu kwa wakulima wengine juu ya umuhimu wa Ushrika afya na kuwataka wachangamkie fursa hiyo adhimu kwao.
Hafla ya utiaji saini hati ya makubaliano ya bima ya Afya kwa wakulima wa miwa baina ya Banki ya CRDB, NHIF, na AMCOS za wakulim wa miwa wilayani kilombero imehudhuliwa na viongozi mbalimbali wa Serikali na AMCOS.
Maafisa wa Banki ya CRDB na Mfuko wa bima ya Afya NHIF wakiwa katika picha ya pamoja (kushoto) ni Meneja wa kanda ya Kati Banki ya CRDB Chabu Mishwaro,(wapili kutoka kushoto) Kaimu Meneja mkuu wa Banki ya CRDB, Wilson Mnzava (watatu kutoka kushoto) ni Mkurugenzi wa huduma za uanachama (NHIF ) Hipoliti Lello(wa mwisho kulia) ni Neema Matiga Afisa masoko huduma kwa wateja NHIF.
Zoezi la utiaji saini ya makubalino ya Bima ya Afya kwa wakulima likiendelea baina ya Banki ya CRDB,NHIF, PAMOJA na AMCOS za wakulima wa miwa Wilayani Kilombero (kushoto) ni Kaimu Meneja mkuu wa Banki ya CRDB, Wilson Mnzava (kulia) kaimu Mkurugenzi wa huduma za uanachama (NHIF) Hipoliti Lello
Kushoto ni Kaimu Meneja mkuu wa Banki ya CRDB, Wilson Mnzava akiwa katika picha ya pamoja na katibu wa chama cha ushirika cha Katurukila baada ya utiaji saini hati ya makubaliano ya Bima ya afya kwa wakulima wa miwa Wilayani Kilombero baina ya Banki ya CRDB,NHIF, na AMCOS.
Kaimu Meneja mkuu wa Banki ya CRDB, Wilson Mnzava akizungumza na viongozi wa vyama vya ushirika (AMCOS) Wilaya ya Kilombero katika hafla ya utiaji saini ya makubaliano ya Bima ya afya kwa wakulima baina ya Banki ya CRDB,NHIF, na AMCOS za wakulima wa miwa.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment