DC JOKATE AZINDUA AWAMU YA PILI YA 'MEET YOUR STAR' YA ZAMARADI MKETEMA, 'TUWASAPOTI WASANII WETU' | Tarimo Blog


Mkuu wa wilaya ya Temeke Jokate Mwegelo akikagua baadhi ya bidhaa zinazopatika katika banda la "Mama kimbo" linalopatikana katika Maonyesho ya Biashara ya Sabasaba "Meet your star" lililoandaliwa na Zamaradi Mketema.
Pichani ni Banda la Taasisi ya The warrior Women ambapo Mkuu wa wilaya ya Temeke Jokate Mwegelo ameweza kutembelea, Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Sabra Machano akijaribu kumuelekeza namna ya utengenezaji wa vinywaji hasa juisi ya Muhogo.
Msanii wa Tamthilia ya "Huba"  Kibibi akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Temeke Jokate Mwegelo  pambo la Nyumbani kama zawadi katika Maonyesho ya Biashara ya Sabasaba Dar es salaam.
Picha ya pamoja ya Mkuu wa wilaya ya Temeke Jokate Mwegelo pamoja na  baadhi  Wasanii ambao wapo katika banda  la "Meet your star" kwa Mwaka huu katika Maonyesho ya Biashara ya Sabasaba Dar es salaam.


Khadija Seif, Michuzi TV

MKUU wa Wilaya ya Temeke, Jokate Mwegelo amempongeza Mtangazaji, Zamaradi Mketema kwa namna ambavyo ameendelea kuwa mbunifu ikiwa ni pamoja na kusaidia kuibua upande wa pili wa wasanii nchini.

DC Jokate ametoa kauli hiyo leo wakati alipotembelea maonesho ya kibiashara ya Sabasaba ambapo amezindua msimu wa pili wa mradi wa 'Meer your Star' yaani kutana na Staa wako uliopo chini ya Zamaradi.

Mradi huo wa Meet your star una lengo la kuwawezesha wasanii mbalimbali nchini kuonesha biashara zao kwenye maonesho hayo ya Sabasaba ambapo pia watapata fursa ya kuonana na mashabiki zao.

Akizungumza katika uzinduzi huo, DC Jokate amempongeza Zamaradi kwa ubunifu huo huku pia akiwasifu wasanii ambapo wamejitokeza kuonesha biashara zao katika maonesho hayo maarufu ya kibiashara barani Afrika.

" Kupitia "Meet your star" unaweza ukakutana na msanii ambaye ulitamani kumuona lakini pia unaweza kujua mbali na sanaa msanii huyo anajishughulisha na kitu gani hivyo ningependa kuona Mashabiki wasiishie kuwaona tu bali waweze kununua bidhaa zao ili kuendelea kupeana moyo.

Nitoe wito kwa wasanii kutumia jukwaa hili kuonesha biashara zao kwani licha ya kuzitangaza na kupata kipato lakini pia zinawaweka karibu na mashabiki zao ambao wamekua wakiwasapoti kila siku," Amesema DC Jokate.

Jokate pia ametoa wito kwa mashabiki wa muziki, filamu na sanaa kwa ujumla kujitokeza kwa wingi kwenye maonesho hayo na hasa kwenye mabanda ya wasanii hao ili kuona na kusapoti kazi za nje ya sanaa za wasanii wanaowapenda.

DC Jokate ameweza kutembelea mabanda ya wafanyabiashara hao ambao ni wasanii na kujionea bidhaa mbalimbali ikiwemo vyakula, vipodozi, nguo pamoja na manukato.

Kwa upande wake Mwanzilishi wa "Meet your star", Zamaradi Mketema amemshukuru DC Jokate kwa kuitikia wito na kuipa thamani tasnia ya Burudani nchini kuanzia Bongomovie, Bongo fleva na Mitindo.

" Tumeweza kuwakutanisha wasanii na mashabiki zao kwa mwaka jana hivyo hivyo kwa Mwaka huu tutakutanisha tena, na tuwashukuru Tantrade wametubeba na wametupa nafasi ya kushiriki maonyesho haya bure hivyo ni fursa sasa wasanii kujikwamua kiuchumi na kutumia jukwaa hili kama chanzo Cha kujitanua kibiashara," Amesema Zamaradi.

Aidha,Mketema amempongeza Mkurugenzi wa Taasisi ya The warrior Women, Sabra Machano kwa kumshika Mkono kwa hali na mali na kuhakikisha "Meet your star" inasimama na inafika katika jamii japo lilikua ni wazo tu ambalo hakutegemea lingefika nafasi ya viongozi kupongeza kama alivyofanya waziri Mkuu Kasim Majaliwa kwa Mwaka 2020.


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2