GERMAN MACHINE YAJIPANGA KUTOA ELIMU YA UCHIMBAJI WA VISIMA VYA KISASA | Tarimo Blog


Moja ya bwawa la samaki la Kisasa linalotengenezwa na Kampuni ya German Machine aquatic.
Muonekano wa bwawa la samaki lililotengenezwa na Kampuni ya German Machine aquatic.

Na Khadija Seif, Michuzi Tv

KAMPUNI ya German Machine aquatic investment yawataka wajasiriamali wadogo na wakubwa kuwekeza katika uchimbaji wa visima vya Kisasa ili waweze Kuboresha ufugaji wa samaki wenye tija na usalama .

Akizungumza na Michuzi Tv Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Jphnson Msuya emeelezab Kampuni hiyo imejikita kwenye utoaji wa huduma za ufugaji wa samaki kwa njia za Kisasa zaidi na uchimbaji wa visima.

"Nawakaribisha sana wafanyabiashara hasa wenye uhitaji wa elimu ya namna gani utaweza kumudu Biashara hii ya ufugaji wa samaki wa Kisasa."

Hata hivyo Msuya ametaja huduma zingine zinazotolewa na Kampuni hiyo ni kutoa mafunzo kwa wajasiriamali ambao wataweza kufaidika na kuingiza kipato kupitia biashara kwa gharama nafuu.

 "Elimu nyingine watakayopata katika banda letu ni pamoja na kujua jinsi ya uchimbaji wa visima, Mabwawa ya Samaki,uuzaji wa vifaranga, utengenezaji wa chakula bora cha samaki pamoja na kutengeneza mitambo ya kumwagilia Mashamba."


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2