Kazi ya Udereva hairidhishwi kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine-Munuo | Tarimo Blog

 

Mwalimu wa VETA Kihonda mkoani Morogoro William Munuo akizungumza na mwananchi aliyetembelea banda la VETA katika Maonesho ya 45 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam.

*Udereva ni kusoma sio kukaa na dereva ni ndio kujua

Na Chalila Kibuda ,Michuzi TV
MADEREVA wa Magari Makubwa wametakiwa kupata mafunzo mara kwa mara kutokana na Teknolojia ya magari inabadilika kila siku ikiwa ni pamoja alama za Usalama Barabarani nazo zinabadilika.

Hayo ameyasema Mwalimu wa Madereva wa Magari Makubwa wa Chuo cha VETA Kihonda mkoani Morogoro William Munuo katika maonesho ya 45 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam, amesema asilimia 95 ya uchumi wa viwanda inategemea madereva kwa ajili ya kusafirisha bidhaa na Mali Ghafi.

Amesema kazi ya udereva ni taaluma na sio kazi ya kuridhishana hivyo madereva wanatakiwa kusoma ili kuweza kusukuma uchumi wa nchi.

Aidha amesema madereva wanaondesha Magari Makubwa wanatakiwa kuendesha kwa muda wa masaa tisa na baada ya hapo wanatakiwa kupumzika kwa ajili ya kuendelea na safari.

Aidha amesema kuwa madereva wa magari makubwa na yale ya abiria hawatakiwi kufanya kazi hiyo wakiwa wamelewa pombe kwani wanaweza kusababisha ajali.

Munuo amesema Chuo kihonda kipo kwa ajili ya kutoa Mafunzo hivyo madereva hawana budi kusoma ili kuweza kufanya kazi hiyo kwa ufanisi.

Amesema kuwa wananchi watembelee banda la VETA na kupata maelezo kuhusiana na kozi hizo

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2