Alberto Cheru wa DIT akimueleza Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Profesa James Mdoe aina za mchanga na kokoto zinazofaa kwenye ujenzi na uhandisi wa Migodi alipotembelea banda la DIT katika maonyesho ya 45 ya biashara ya kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Dar es Salaam.
Mbunifu kutoka chuo cha DIT, Dotnata Ntunga, akimuelezea Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Profesa James Mdoe namna mfumo ambao unawekwa kwenye kifaa cha kutunzia wa watoto uyakavyokuwa unasaidia wauguzi kujua hali ya mtoto hata akiwa mbali na chumba cha mtoto.Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Profesa James Mdoe(kulia) akipata maelezo kutoka kwa mbunifu kutoka chuo cha DIT, Joel Ngashwai aliyebuni kifaa cha kufundishia madaktari, CPR. Wakati waziri huyo alipotembelea banda ya DIT katika Maonesho ya 45 ya biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere eneo la barabara ya Kilwa Dar es Salaam.
Na Karama Kenyunko Michuzi TV
NAIBU Katibu Mkuu wa Sayansi na Teknolojia, Profesa James Mdoe amesema Wizara hiyo itasaidia kazi za ubunifu zinazofanya na wanafunzi na wakufunzi wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) kutoka kwenye maonesho na kwenda kutatua changamoto katika jamii.
Pia ameishauri DIT kuendelea kujitangaza ili iweze kupata wanafunzi wengi kwenye programu za masters kwa sababu wanafunzi ni wachache, lakini kuna watu wanauhitaji wa kufika katika hatua hiyo.
Profesa Mdoe amesema hayo leo Julai 6, 2021 alipotembelea banda la DIT katika Maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa 'Sabasaba' yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere Dar es Salaam.
Amesema wao kama wizara watachukua changamoto za taasisi hiyo ili vifaa vilivyobuniwa viweze kuondoka kwenye hatua waliyopo sasa hivi ili vifike hatua vikatatue changamoto ambazo zinapaswa kutatuliwa kwenye jamii.
"Nimeona kijana amebuni mfumo wa kuwatunza watoto njiti, ni ubunifu mzuri kwasababu nesi anakaa ofisini lakini anapata taarifa kuna mtoto anahitaji huduma...pia nimeona kijana amebuni mfumo wa kutengeneza vifaa vya kufundishia wanafunzi madaktari na vingine hizi ni bu nm ifu nzuri na tutazifanyia kazi' amesema Profesa Mdoe.
Aidha, Profesa Mdoe ameipongeza DIT kwa ufundishaji mzuri wa vitendo kwani mafunzo yao ni ya viwandani, mwanafunzi anafundishwa darasani lakini anakwenda pia viwandani kujifunza zaidi.
Aidha Profesa Mdoe amewashauri wabunifu kutumia atamizi za DIT kwani ni mahali ambapo mbunifu mwenye wazo lake anaweza kwenda pale akawekewa mazingira ya kuweza kulifanyia kazi kufika kwenye huduma au bidhaa ambapo muda si mrefu tutapata matunda mazuri kutoka kwenye hizo atamizi.
"Wabunifu hasa is waliopo Dar es Salaam ni rahisi kufika DIT wakajiandikisha na kupeleka mawazo yeo ambapo watawekewa mazingira wezeshi hata nayo wa zaidi wao pamoja na jamii kwa ujumla. " amesema Profesa Mdoe
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment