Na Marco Maduhu, Shinyanga
KLABU ya Mazoezi Polisi Jamii Fitness Center ya mjini Shinyanga (PJFCS,) ambayo ipo chini ya Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga, imetoa msaada wa mitungi 16 ya Hewa ya Oksijeni katika Hospitali ya Rufaa mkoani humo, ili kusaidia wagonjwa wenye changamoto ya upumuaji.
Akizungumza leo wakati wa kukabidhi mitungi hiyo Mwenyekiti wa Klabu hiyo Sadick Kibira amesema, wameamua kuchangishana fedha kwa kila mwanachama, na kufikisha kiasi cha fedha Sh. 928,000 na kununua Mitungi hiyo 16 ya hewa ya Oksijeni.
Amesema Klabu hiyo ya mazoezi kila mwaka katika msimu wa sherehe za Sabasaba, huwa wanaadhimisha siku hiyo kwa kutoa misaada mbalimbali kwa wahitaji pamoja na kuchangia damu, ambapo kwa mwaka huu wameamua kutoa msaada wa mitungi 16 ya hewa ya Oksijeni katika Hospitali ya Rufani mkoani Shinyanga.
“Tumetoa mitungii hii ya hewa ya Oksijeni 16 katika Hospitali ya Rufaa mkoani Shinyanga na kuchangia damu, ambapo Mitungi hii itasaidia kwa kiasi kikubwa kuhudumia wagonjwa wenye changamoto ya upumuaji,” Amesema Kibira.
Kwa upande wake Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Mfaume Salum, amesema msaada wa Mitungi hiyo ya hewa ya Oksijeni 16, imesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza changamoto ya upungufu wa mitungi hospitalini hapo.
Vilevile Mnadhimu wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga, Joseph Paul akizungumza kwa niaba ya Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga George Kyando, ameipongeza Klabu hiyo kwa kutoa msaada huo wa mitungi ya hewa ya Oksijeni, na kutoa wito kwa wadau wengine kuiga mfano huo.
Wanachama wa Klabu ya Mazoezi ya Polisi Jamii Fitness Center wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mitungi ya Hewa ya Oksijeni katika Hospitali ya Rufaa mkoani Shinyanga.
Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga DK. Mfaume Salum, akizungumza mara baada ya kupokea msaada wa mitungi hiyo 16 ya hewa ya Oksijeni.
Mwenyekiti wa Klabu ya Mazoezi ya Polisi Jamii Fitness Center Sadick Kibira , akizungumza mara baada ya kumaliza kukabidhi Mitungi 16 ya Hewa ya Oksijeni katika Hospitali ya Rufaa mkoani Shinyanga.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment