MAKAMU WA RAIS AFANYA MAZUNGUMZO NA WAZIRI WA BIASHARA WA UFARANSA | Tarimo Blog



Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango akimkabidhi zawadi ya mchoro wa Picha ya wanyama watano wakubwa (Big Five) wanaopatikana nchini Tanzania waziri anaeshughulikia masuala ya Biashara ya Kimataifa na Uchumi  Mhe. Franck Riester Paris Nchini Ufaransa Julai 2, 2021.


Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango akiwa katika mazungumzo na waziri anaeshughulikia masuala ya Biashara ya Kimataifa na Uchumi Mhe. Franck Riester Paris Nchini Ufaransa Julai 2, 2021.



Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango akimkabidhi zawadi ya mchoro wa Picha ya wanyama watano wakubwa (Big Five) wanaopatikana nchini Tanzania waziri anaeshughulikia masuala ya Biashara ya Kimataifa na Uchumi Mhe. Franck Riester Paris Nchini Ufaransa Julai 2, 2021.

**************************

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango amekutana na kufanya mazungumzo na waziri anaeshughulikia masuala ya Biashara ya Kimataifa na Uchumi Mhe. Franck Riester Paris Nchini Ufaransa hii leo Julai 2, 2021.

Katika mazungumzo yao, pande zote mbili zimekubaliana kuendeleza ushirikiano mzuri ambao umedumu kwa muda mrefu hususan katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kuendelea kuimarisha uhusiano wa biashara kati ya pande mbili. Kupitia Waziri huyo Serikali ya Ufaransa imeahidi kuongeza kiwango cha fedha kwa ajili ya ufadhili wa miradi ya maendeleo katika sekta ya miundombinu, kilimo, afya na maji.

Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Samwel Shelukindo, Katibu Mkuu wizara ya Afya – Idara kuu ya maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk N Mbarouk.


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2