MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Alhaj Othman Masoud Othman, leo Ijumaa (Julai 9) amejumuika na ndugu, jamaa na wanafamilia katika maziko ya mama wa msaidizi wake.
Marehemu Bi. Msima, aliyefariki usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake Muembe Makumbi, ni mama wa Bwana Khamis Mikidadi, ambaye ni miongoni mwa wasaidizi wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.
Marehemu amezikwa leo kijijini kwao Patanani kilichopo Bumbwini Mafufuni, Wilaya ya Kaskazini B katika Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Mheshimiwa Othman, ambaye aliambatana na mke wake Bi. Zuhura Kassim Ali, kwa pamoja wametoa mkono wa pole kwa familia ya Bwana Khamis Mikidadi wakiwasihi wawe na subra katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mzazi wao.
Wakati huo huo, Makamu huyo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar aliungana na waumini wenzake wa dini ya Kiislamu katika ibada ya Sala ya Ijumaa iliyosaliwa katika Msikiti Makuti uliopo Jang’ombe, Mjini Unguja.
Akizungumza na waumini mara baada ya sala hiyo, Alhaj Othman amewasisitiza kuendelea kuwa wamoja kwa kupendana na kushirikiana katika mambo ya kheri na kufuata nyayo za Kiongozi wa Umma, Mtume Muhamad (S.A.W), na pia kuwaunga mkono viongozi wao.
“Nawaomba tuyazingatie maneno ya khatibu wetu, Sheikh Mudiru, ya kuwapenda na kuwaunga mkono viongozi wetu na kuepuka chokochoko na mitafaruku ili kujiepusha na machafuko.” Alisema Alhaj Othman.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment