Mkuu wa wilaya ya Babati ahimiza wananchi tahadhari UVIKO 19. | Tarimo Blog

 Na John Walter-Babati

Mkuu wa wilaya ya Babati Lazaro Twange ameyaomba mashirika binafsi yaliyomo wilayani humo kuendelea kuiunga mkono serikali katika kutoa elimu kwa Wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya wimbi la tatu la UVIKO 19 na kutoa vifaa kinga katika maeneo hatarishi.

Ameyazungumza hayo leo julai 28,2021 akizungumza na NGOs ili kujua kazi zao na  changamoto zinazowakabili,mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano halmashauri ya mji wa Babati.

Twange amesema mashirika hayo kwa kuwa yanafanya kazi na watu yana nafasi katika kuhimiza wananchi kuchukua tahadhari za kujikinga na mlipuko wa ugonjwa huo.

Akieleza mikakati ya kujikinga na maradhi hayo, mkuu wa wilaya amesema wamejipanga kudhibiti mikusanyiko yote isiyokuwa ya lazima huku wataalamu wa afya wakiendelea kutoa elimu kwa njia mbalimbali.

Kwa upande wa mashirika hayo yameahidi kuendelea kuiunga mkono serikali ili kukabiliana na janga hilo la Korona kwa kuchukua tahadhari zinazopaswa wakati wote.


 

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2