Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mheshimiwa Suleiman Kakoso, akitoa salamu za pole kwa familia ya marehemu Mhandisi Patrick Mfugale, katika Hospitali ya Benjamin Mkapa, jijini Dodoma alipofika hapo kutoa heshima za mwisho.
Jeneza lililobeba mwili wa aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Marehemu Mhandisi Patrick Mfugale, likiwasili eneo maalum katika Hospitali ya Benjamin Mkapa, jijini Dodoma kwa ajili ya kufanyiwa ibada na kupewa heshima ya mwisho na viongozi wa Serikali, watumishi wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi na waombolezaji wengine.
Viongozi mbalimbali, watumishi wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi pamoja na wafanyakazi wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), wakitoa heshima zao za mwisho kwa aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), katika Hospitali ya Benjamin Mkapa, jijini Dodoma.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment